Misingi mitatu makala namba No.9

https://t.me/fawaidussalafiyatz

📖 ثلاثة الأصول 📖

MISINGI MITATU

◾وأعظم ما أمر الله به التوحيد وهو إفراد الله بالعبادة
◾ وأعظم ما نهى عنه الشرك وهو دعوة غيره معه

Na kubwa zaidi aliloamrisha Allah ni kupwekesha , na huko (kupwekesha ) ni kumjalia Allah mmoja katika ibada .Na kubwa zaidi alilolikataza Allah ni ushirikina nao ni kumuabudia mwengine pamoja na (Allah).

↩والدليل قوله تعالى

( واعبدوا الله ولا تشركوا به شيئا)

Na dalili (ushahidi) ni kauli yake (Allah) aliyetukuka :

(Na muabuduni Allah na wala msimshirikishe na chochote).

النساء ٣٦

Maelezo:

Maana iliyokusanya zaidi katika kumpwekesha Allah ni:

” kumpwekesha Allah katika yale ambayo anahusika nayo (yeye) peke yake”

Na huko kumpwekesha Allah kumegawanyika sehemu tatu :

1-Kumpwekesha Allah katika matendo yake, na matendo makubwa katika hayo :
1- Kumiliki 2- kutoa riziki ,3-kuumba ,4-kuendesha mambo .

2-Kumpwekesha Allah katika ibada, yaani kumuabudia Allah pekee na kutomuabudia yeyote pamoja na Allah mfano ukaomba mizimu,au ukamuomba maiti akutatulie shida zako kwa sababu kuomba ni ibada hivyo ni wajibu maombi yote umuelekezee Allah ukielekeza kwa mwengine umemshirikisha Allah.

3- Kumpwekesha Allah katika sifa na majina ,kwa kuthibitisha majina na sifa ambazo amejisifu kwazo katika kitabu chake au amemsifu kwazo Mtume swala na salam za Allah ziwe juu yake ,na kumkanushia zile alizojikanushia au alizomkanushia Mtume bila kupindua maana, na wala kuacha kuthibitisha ,na bila ya kutafuta namna namna na bila kufananisha .

Ushirikina ni kunyume na kumpwekesha Allah, nao “Ni kumfanyia Allah mshirika katika matendo yake na ibada zake na majina na sifa zake ”

Na ushirikina ndiyo dhambi kubwa zaidi na vigawanyo vyake ni aina mbili:

1- Ushirikina mkubwa ambao humtoa mtu katika uislamu mfano : kumchinjia asiyekuwa Allah kama vile ukachinja kwa ajili ya zindiko au shetani kwa kujikurubisha kwa huyo unayemchinjia ,na yule atakayekufa na aina hii ya ushirikina atadumu motoni milele,

2-Ushirikina mdogo nao ni kila tendo au neno ambalo limetajwa na sheria kua ni ushirikina lakini halimtoi mtu katika uislam.

Amesema Allah- aliyetukuka-:

ۖ إِنَّهُ مَنْ يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنْصَارٍ

“Hakika hali ilivyo mwenye kumshirikisha Allah,basi hakika Allah amemzuilia pepo na mafikio yake ni motoni na hawana madhwaalimu wa kuwanusuru”

النساء ٧٢

Usia :

Tambua ewe muislam -Allah akurehemu -kuwa amri ya kwanza ambayo Allah aliwaamrisha waja ni tauhidi yaani kumuabudia peke yake na katazo la mwanzo ambalo alilowakataza ni ushirikina.

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Ramadhani 15, 1442H ≈ April 27, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *