Misingi mitatu na dalili zake.

➡️makala namba (18)

◽ودليل الرغبة
◽والرهبة
◽والخشوع

Na dalili ya shauku,na kuogopa,na kunyenyekea (kuwa ni katika ibada)

🌱قوله تعالى:

{إِنَّهُمْ كَانُواْ يُسَٰرِعُونَ فِى ٱلْخَيْرَٰتِ وَيَدْعُوnنَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُواْ لَنَا خَٰشِعِينَ‎}

Ni kauli yake (Allah) aliyetukuka :

{Hakika wao walikuwa wepesi wa kutenda mema,na wakituomba kwa shauku na khofu .Nao walikuwa wakitunyenyekea}

الأنبياء ٩٠

Maelezo yanayotokana na sherehe za wanavyuoni:

Shauku : Ni kupenda kukifikia kitu kinachopendwa

Hofu :Makusudio ya hofu hapa ni hofu inayoambatana na matendo

Kunyenyekea :Ni kujidhalilisha kwa Allah kwa kujisalimisha katika makadirio yake ya kisheria na ya kiulimwengu.

Katika aya hii Allah anawasifu waja wake watukufu ambao ni manabii na Mitume -amani iwe juu yao -kwamba wao wanamuabudu Allah kwa shauku ya kupata yale yaliyoko kwa Allah na kutumaini thawabu zake pamoja na kuogopa adhabu zake na kuogopa athari ya dhambi zao.

Na muumin inatakikana amuelekee yaani amuabudu Allah baina ya kuogopa na kutaraji kwa maana amuabudu kwa kusanya ibada hizi mbili :Kuogopa na kutaraji

na mitume swala na salam ziwe juu yao wamekusanya sifa hizi tatu ambazo ni katika aina za ibada.

Na vile vile Allah amewasifu hawa Manabii na Mitume na maadamu amewasifu basi hizo ni katika ibada zinazoridhiwa na Allah ,na yeyote atakayemfanyia ibada hizo asiyekuwa Allah basi atakuwa amemshirikisha Allah mfano wale wenye kuwaabudia maiti wanapokuwa katika makaburi ya hao wanaowaabudia huwa na unyeyekevu wa hali ya juu zaidi ya vile wanavyosimama katika swala zao mbele ya Mola wao! ,na bila shaka huu ni katika ushirikina mkubwa unaomtoa mtu katika uislamu.

Na pia ndani ya sifa/ibada hizi kuna kuwakosoa masufi yaani watu wa twariqa ambao wanasema :

“Sisi hatumuabudu Allah kwa kutaka thawabu wala kuogopa adhabu zake na hakika si vinginevyo tunamuabudu kwa kumpenda tu”

Haya maneno si ya sawa kwa sababu Mitume -amani iwafikie-walimuabudia Allah kwa kumpenda na kumuogopa na wao ndio viumbe waliokamilika zaidi.

Mpitiaji: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 19, 1443H ≈ Feb 20, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *