➡️ Makala namba ( 19)
↩️ودليل الخشية قوله تعالى :
🌱{فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِي } البقرة
(١٥٠)
Na dalili ya kuogopa ni kauli yake Allah aliyetukuka:
“Basi msiwaogope wao lakini niogopeni mimi”
↩ودليل الإنابة قوله تعالى :
🌱{وَأَنِيبُوٓاْ إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَأَسْلِمُواْ لَهُۥ}
(الزمر ٥٤).
Na dalili ya kurejea ni kauli yake Allah aliyetukuka:
“Na rejeeni kwa Mola wenu Mlezi na nyenyekeeni kwake”.
Maelezo yanayotokana na sher’he za wanavyuoni :
Na miongoni mwa ibada ambazo Allah -aliyetukuka – ameziamrisha ni :
Uwoga na uwoga unaokusudiwa hapa ni ule uwoga uliojengeka juu ya kujua ukubwa wa yule unayemuogopa na ukamilifu wa uwezo wake .
amesema Allah aliyetukuka:
ۗ إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ ۗ
{Kwa hakika wanaomuogopa Allah miongoni mwa waja wake ni wale wenye elimu)}
Surat Faatwir aya ya ( 28).
Hapa wanakusudiwa wanachuoni wanaojua ukubwa wa Allah na ukamilifu wa uwezo wake, kwa hiyo aina hii ya kuogopa imehusisha zaidi elimu kuliko aina nyengine.
Kurejea:
Maana yake ni kurudi kwa Allah kwa kusimama imara katika kumtii na kujiepusha na kumuasi, na huko kurejea kwa Allah kunakaribiana na toba isipokua kurudi kwa Allah kuna maana iliyojificha zaidi, kwa sababu mwenye kurejea huhisi amejiegemeza kwa Allah na amekimbilia kwake.
Na huku kurudi kwa Allah si kurudi tuu bali ni kurudi kwa moyo pamoja na kujifungamanisha kwa Allah na kutaraji kwake
Na moyo unaorudi kwa Allah ni ule uliosimama katika aina kadhaa za ibada za moyo, miongoni mwa hizo ni kutaraji, kuogopa, kupenda n.k
Basi Allah ametuamrisha turudi kwake na kwakuwa ametuamrisha maana yake analipenda hilo la sisi kurudi kwake na analiridhia kwa yule atakayelitekeleza na hii ni dalili kuwa kurudi kwa Allah ni ibada.
Na pale aliposema :
“Na Jisalimisheni kwake”
makusudio ya kujisalimisha kwa Allah hapa ni kujisalimisha katika hukumu za Allah za kisheria kwa sababu kujisalimisha kwa Allah kumegawanyika sehemu mbili:
1️⃣-Kujisalimisha katika hukumu za Allah za kiulimwengu kwa maana kila analolikadiria Allah lazima litokee na kila lililokadiriwa na Allah kwa kiumbe lazima limfike apende asipende na hili linakusanya vyote vilivyopo mbinguni na ardhini muumini na
kafiri,mwema na muovu.
amesema Allah aliyetukuka:
أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ
{ Je wanataka dini isiyokua ya Allah na hali ya kuwa kila kilichomo Mbinguni na Ardhini kinamtii yeye kikipenda kisipende? na kwake vitarejeshwa vyote}•
Al-imraan (83)
2️⃣-Kijisalimisha katika hukumu za Allah za kisheria kama vile kutekeleza ibada mbali mbali, na hii ni maalumu kwa yule anayemtii Allah yaani muislamu, kama vile mitume na wenye kuwafuata hao mitume kwa wema.
Mpitiaji : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 3, 1443H ≈ Mar 6, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•