Makala namba ( 27)
↩️ وهو ثلاث مراتب
Na huo (uislamu ni) daraja tatu:
🌱 الاسلام
🌱 والإيمان
🌱 والإحسان
وكل مرتبت لها أركان
1️⃣ Uislam,
2️⃣ na imani,
3️⃣ na ihsani
Na kila daraja lina nguzo.
✍️Sherhe inayotokana na wanachuoni mbalimbali:
ೄྀ࿐ ೄ࿐ೄྀ࿐ ೄ࿐ೄྀ࿐ ೄ
Daraja za dini ni tatu baadhi ya hizi daraja zipo juu zaidi kuliko nyengine nazo ni kama alivyozitaja sheikh hapa :
🌱 Kwanza:
Uislamu,
🌱kisha imani ,
🌱kisha ihsani .
1- Daraja la Uislamu ni pana zaidi kwa maana Uislamu ni mpana zaidi, na daraja la imani ni finyu zaidi kuliko uislamu na daraja la ihsani ni finyu zaidi kuliko Imani.
Kwa kuweka wazi zaidi tunasema hivi:
Uislamu ni kama duara kubwa ambalo ndani yake kuna duara la imani ambalo ni dogo kuliko duara la Uislamu na kuna duara la ihsani ambalo ni dogo zaidi kuliko la imani, mtu anaweza akatoka katika duara la imani lakini akabakia katika duara la Uislamu kwa maana mtu anaweza asiwe ni muumini lakini akabakia kuwa muislamu .
Kwa hiyo daraja la Uislamu ni pana zaidi hata wanafiki wanaingia ndani yake, kama wanafiki wakifuata Uislamu kwa wazi na wakajilazimisha nao kwa wazi wakaswali pamoja na waislamu na wakafanya matendo ya uislamu kwa uwazi basi wataitwa waislam, na watapitishiwa hukumu za uislam katika dunia, na watapewa yale wanayopewa waislam ,na watawajibika kuyafanya yale yanayowawajibikia waislam lakini wao huko Akhera watakuwa katika kina cha chini zaidi katika moto,kwa sababu wao hawana imani bali uislamu wao ni ule wa kimuonekano tu na kidhahiri .
2- Na daraja la pili ni daraja la imani na hao waumini wanatofautiana katika daraja zao na daraja zao ni tatu nazo ni :
1️⃣ Daraja la wale waliokurubishwa kwa Allah, na hawa ni wale waliotekeleza mambo ya faradhi na sunna na wakajiepusha na ya haramu na ya karaha (yanayochukiza) na hawa ndio wenye daraja za juu kabisa wataingia peponi mwanzoni kabisa bila ya kuhesabiwa matendo yao wala kuadhibiwa.
2️⃣ Daraja la wale wa katinakati hawa wao ni wale waliotosheka na faradhi tu yaani hawana sunnah lakini wanajiepusha na ya haramu ila hawajiepushi na yale ya karaha na hawa wataingia peponi mwanzoni kabisa bila ya kuhesabiwa wala kuadhibiwa ila daraja lao sio sawa na ya wale waliokurubishwa.
3️⃣ Daraja la waumini waliyofanya madhambi makubwa ambayo si ya ushirikina wala ukafiri hawa wanaitwa ni waumini waovu au waumini waliopungukiwa na imani .
Na makundi haya matatu Allah -aliyetukuka- ameyataja katika kauli yake ifuatayo:
{ثُمَّ أَوْرَثْنَا ٱلْكِتَٰبَ ٱلَّذِينَ ٱصْطَفَيْنَا مِنْ عِبَادِنَا ۖ فَمِنْهُمْ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِۦ وَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌ وَمِنْهُمْ سَابِقٌۢ بِٱلْخَيْرَٰتِ بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَضْلُ ٱلْكَبِيرُ}•
Kisha tumewarithisha kitabu wale ambao tumewachagua miongoni mwa waja wetu,
Basi wako miongoni mwao wanaodhulumu nafsi zao, Na wako wa kati na kati . na wako wanaokwenda mbele kabisa katika mambo ya kheri,kwa idhini ya Allah. hiyo ndiyo fadhila kuu.
جَنَّٰتُ عَدْنٍۢ يَدْخُلُونَهَا يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍۢ وَلُؤْلُؤًا ۖ وَلِبَاسُهُمْ فِيهَا حَرِيرٌ
Pepo za milele wataziingia,humo watapambwa vikuku vya dhahabu,na lulu,na nguo za humo zitakuwa za hariri .
سورة فاطر 32-33 .
Katika aya hizi mbili za suratu Fatir Allah amewagawanya waislamu katika makundi matatu na akasema kuwa yote yataingia peponi hata wale waislamu waliokuwa wakimuasi Allah kwa kufanya madhambi hata makubwa au kwa kuacha kutekeleza wajibu maadamu wamekufa hali ya kuwa hawamshirikishi Allah na hata kama wataingia motoni lakini watatolewa na kuingizwa peponi .
3- Na daraja la tatu katika daraja za Uislamu ni daraja la ihsani :
Ihsani maana yake ni kufanya matendo vizuri, nako kumegawanyika mara mbili :
1- Kuwafanyia ihsani (wema) viumbe .
2- Kufanya ihsani katika kumuabudia Allah, na ihsani katika kumuabudia Allah kuna daraja mbili:
(a) Daraja la kushuhudia : Ni muislamu kumuabudu Allah kana kwamba unamuona kwa macho yake kwa sababu ya yakini aliyokuwa nayo na ikhlas iliyopo katika moyo wake, na bila shaka tunajua kuwa Allah haonekani hapa duniani lakini muislamu atapofanya ibada katika sura hii kwa kuuhudhurisha katika moyo wake kana kwamba yupo mbele ya Allah bila shaka atajitahidi kuifanya hiyo ibada kwa uzuri zaidi na kuikamilisha .
(b) Daraja la kuchunga (kuogopa) : Kama muislamu hakuweza kulifikia daraja hilo la kwanza basi aliendee daraja hili la pili ambalo ni kumuabudu Allah hali ya kujua kuwa Allah anamuona, na mja anatakiwa ahudhurishe katika moyo wake hofu ya Allah,lakini daraja la kwanza la ihsani lipo juu zaidi kuliko daraja hili la pili.
Hii ndiyo nguzo ya ihsani (wema) nayo ni daraja kubwa zaidi ya uchamungu Kama alivyosema ibn -lQayyim- Allah amrahamu-:
(منزلة الإحسان هي لب الإيمان وروحه وكماله).
“ Daraja la ihsani hilo ndiyo hakika ya imani na roho yake na ukamilifu wake ”
مدارج السالكين
Mfasiri Ummu Muhammad.
Imepitiwa na : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo mosi 26, 1445H ≈ May 5, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•