Misingi mitatu na dalili zake .

➡️ Makala namba (23)

↩️ودليل الذبح قوله تعالى :

Na dalili ya kuchinja (kuwa ni ibada) ni kauli yake Allah aliyetukuka-:

🌱{قُلْ إِنَّ صَلَاتِى وَنُسُكِى وَمَحْيَاىَ وَمَمَاتِى لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ‎}

🌱{لَا شَرِيكَ لَهُۥ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلْمُسْلِمِينَ‎}.

(سورة الأنعام ١٦٢_١٦٣)

{{ Sema :”Hakika swala zangu na kuchinja kwangu (na ibada zote ni haki ya Allah ) na uzima wangu, na kufa kwangu;zote ni milki ya Allah muumba wa walimwengu wote }}

{{ Hana mshirika wake na haya ndiyo niliyoamrishwa,na mimi ni wa kwanza wawaliyojisalimisha kwa Allah }}

↩️ ومن السنة :

Na (dalili) kutoka katika sunnah :

🌱« لعن الله من ذبح لغير الله »

{{ Allah amemlaani anayemchinjia asiyekua Allah }}.

Maelezo yanayotokana na sherhe za wanachuoni mbalimbali:

ೄྀ࿐ ೄ࿐ೄྀ࿐ ೄ࿐ೄྀ࿐ ೄ

Kuchinja: maana yake ni kutoa roho kwa kumwaga damu kwa sura maalum , na kuchinja kumegawanyika sehemu nne :

1️⃣ Uchinjaji wa ibada kwa maana mchinjaji anakusudia kumtukuza yule anayemchinjia, na kujidhalilisha kwake na kujikurubisha kwake, na uchinjaji huu hautakiwi uwe isipokuwa kwa Allah kwa namna aliyoiweka Allah na mwenye kumchinjia asiyekuwa Allah uchinjaji huu basi huyo amemshirikisha Allah ushirikina mkubwa kama alivyotaja sheikh-Allah amrahamu- hapo juu na amesema imamu Nawawiy -Allah amrahamu- :

نص عليه الشافعي ، واتفق عليه أصحابنا ،

Amelitaja hilo Shafi na wameafikiana watu wetu ,

فإن قصد مع ذلك تعظيم المذبوح له غير الله تعالى والعبادة له كان ذلك كفرا ،

Kama akikusudia pamoja na huko (kumchinjia asiyekuwa Allah) kumtukuza anayemchinjia asiyekuwa Allah -aliyetukuka- na kumuabudia basi litakuwa (tendo) hilo ni ukafiri,

فإن كان الذابح مسلما قبل ذلك صار بالذبح مرتدا ،

Na kama mchinjaji alikuwa ni muislamu kabla ya hapo (atakuwa) ameritadi kwa (kule) kuchinja .

شرح مسلم ١٤١/١٣

2️⃣ Kuchinja kwa ajili ya kula, au kuuza hiyo
nyama na mfano wa hayo na hili ni halali kwa sababu mchinjaji hakuchinja kwa ajili ya kujikurubisha na kumtukuza yeyote ,isipokuwa amechinja kwa haja ya kupata nyama na kula au kuuza .

3️⃣ Kuchinja kwa sura ya furaha au kwa munasaba wa ndoa au kuhamia nyumba mpya au kumkirimu mgeni, na yanayofanana na hayo, bila shaka huu ni uchinjaji kwa ajili ya kudhihirisha furaha kwa kile alichokipata na hakuna ubaya wa uchinjaji huu kwa sababu hakuna ndani yake kumtukuza yeyote wala kujikurubisha kwake na tena kuna muda uchinjaji huu unaweza ukawa ni suna au wajibu :

Mfano mtu akachinja kwa ajili ya kuwakirimu wageni kwa sababu kuna wanachuoni wengine wanaona kuwa kumkirimu mgeni ni wajibu kwa muda wa siku mzima yaani usiku na mchana , na wengine wanaona ni sunnah , kama alivyosema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-:

«مَنْ كَان يُؤمِن بِاللهِ وَاليَومِ الآخِرِ فَلْيُكْرِم ضَيفَه..“

“Yule aliyemuamini Allah na siku ya mwisho basi amkirimu mgeni wake ” .

4️⃣ Kuchinja kwa ajili ya kuitoa sadaka nyama kwa mafakiri na masikini na wanaohitaji bila shaka tendo hili linazingatiwa kuwa ni sunna na linaingia katika ibada.

FAIDA :

Ibada ya kuchinja imekusanya ibada zinazoonekana na ibada za kimoyo , ibada zinazoonekana nazo ni : Kutingisha mkono kwa wakati wa kuchinja na kuchezesha ulimi kwa kumtaja Allah .

Na ibada za kimoyo nazo ni :

1- Kumnyenyekea Allah

2- Kumtukuza

3- Kutaraji kutoka kwa kwa Allah wakati wa kuchinja .

4- Kutaka baraka kwa kuchinja kwake kwa ajili ya Allah .

Imepitiwa na : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Safar 8, 1444 H ≈ September 5 2022 M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *