Makala namba (25)
2️⃣ الأَصْلُ الثَّانِي:
↪️ Msingi wa pili:
🌱مَعْرِفَةُ دِينِ الإِسْلامِ بِالأَدِلَّةِ
Ni kuijua dini ya kiislamu kwa dalili.
✍️Sherhe inayotokana na wanachuoni mbalimbali:
ೄྀ࿐ ೄ࿐ೄྀ࿐ ೄೄྀ࿐ ೄ࿐ೄྀ࿐
Pindi alipomaliza Shekh -Allah amrehemu- kubainisha kuutambua msingi wa kwanza ambao ulikua ni kumtambua Allah -aliyetukuka na kushinda- akahama na kuelekea katika kuelezea msingi wa pili nao ni kuijua dini ya kiislamu kwa dalili na ufafanuzi wake ni ufuatao :
Aliposema :
“kuijua dini ya kiislamu kwa dalili”
Sheikh anakusudia kuwa kuijuwa dini ya kiislamu hakuwi kwa kuiga, bali dini hujulikana kwa dalili kutoka katika Quran na sunna kwa maana hadith sahihi .
Ama mwanadamu ambaye haijui dini yake kwa elimu, kwa maana haiamini hii misingi mitatu kwa elimu bali yeye anawaiga watu tu na akawa anafuata kama bendera anaiga tu basi mtu huyu anazingatiwa kuwa haijui dini yake na anaogopewa kuwa atakapoulizwa kaburini kwake aseme :
“Haah ! Haah! sijui niliwasikia watu wakisema kitu na mimi nikasema”.
Basi ni wajibu mtu aijue dini yake kwa dalili kutoka katika kitabu na sunna za Mtume wake -swala na salam za Allah ziwe juu yake na hawezi kuijua hii dini ila kwa kusoma na tuliashiria huko nyuma kuwa makusudio ya kuwa na elimu ya misingi hii mitatu ni mtu kufahamu dalili za misingi hii mitatu na kuziamini na kuzifanyia kazi, na wala si lazima kuhifadhi akawa anauwezo wa kuzileta pindi aulizwapo.
Mfasiri: Ummu Muhammad
Imepitiwa na : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo mosi 23, 1445H ≈ May 2, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•