👈فمن صرف شيئا من أنواع العبادة لغير الله فهو
◾مشرك
◾ كافر
Basi yeyote atakayepeleka chochote katika aina za ibada kwa asiyekua Allah basi (mtu)huyo ni mshirikina Kafiri
والدليل قوله تعالى:
{ وَمَن يَدْعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ لَا بُرْهَٰنَ لَهُۥ بِهِۦ فَإِنَّمَا حِسَابُهُۥ عِندَ رَبِّهِۦٓ ۚ إِنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلْكَٰفِرُونَ}
Na dalili ni kauli yake Allah aliyetukuka:
{Na atakayemuomba- pamoja na Allah- Mungu mwengine, yeye hana hoja ya (jambo) hili; basi hakika si vinginevyo hisabu yake iko kwa Mola wake. Hakika hali ilivyo hawafaulu Makafiri}.
Suratul-Muminun (117)
♦وفي الحديث:
«الدُّعَاءُ مُخُّ الْعِبَادَةِ».
Na katika hadithi:
(Dua ni msingi wa ibada)
⏪والدليل قوله تعالى:
وَقَالَ رَبُّكُمُ ٱدْعُونِىٓ أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِى سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ
Na dalili ni kauli yake Allah aliyetukuka:
{Na amesema Mola wenu mlezi: Niombeni nitakujibuni. Kwa hakika wale ambao wanajitia kiburi kwa kuacha kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu hali ni madhalili}
Suratul-ghafir : 60
Maelezo yanayotokana na sherehe mbalimbali:
Makala hii ina mafungamano na makala iliyopita katika kubainisha kuwa ibada ni haki ya Allah,
baada ya kutaja miongoni mwa aina za ibada kwa ujumla ,kisha shekh -Allah amrehemu- akasema:
Atakayepeleka chochote katika aina za ibada kwa asiyekua Allah ni mshirikina na ni kafiri, makusudio ya ushirikina hapa ni ushirikina mkubwa ambao unamtoa mtu katika Uislam.
Na ushirikina una vigawanyo viwili:
1- Ushirikina mkubwa ambao humtoa mtu katika uislamu : Mfano kumchinjia asiyekua Allah au ukaweka nadhiri kwa asiyekua Allah, au kuwaomba maiti, au wasiokuwepo, n. k
2- Ushirikina mdogo ambao ni katika madhambi mazito na makubwa zaidi lakini aina hii ya ushirikina haimtoi mtu katika uislamu mfano:
Kuapa kwa asiyekua Allah, au kujionesha katika ibada hali ambayo huwenda ikamtokea muumini, kuvaa hirizi kwa kuamini kuwa hiyo hirizi ni sababu ya kupona maradhi au kukingwa na mabalaa na kuamini kuwa mponyaji ni Allah na anayelinda ni Allah, ama akiamini kuwa hiyo hirizi inaponya na kulinda kwa dhati yake bila shaka huo ni ushirikina mkubwa unaomtoa mtu katika uislamu.
Na kuna baadhi ya wanawavyuoni wanaugawa ushirikina sehemu tatu na kigawanyo cha tatu ni :
Ushirikina uliojificha : Na mfano wake ni kama kujionesha kidogo ,na hapa wanasema kujionesha kidogo wanakusudia kuwa kujionesha kukubwa ni katika sifa ya wanafiki ambao wao ibada zao zote huzifanya ili watu wawaone, ama muumini hufanya kwa ajili ya Allah lakini huwenda ikamjia hiyo hali katika baadhi ya nyakati.
Na watu wamegawanyika sehemu tatu katika dua:
1-Kuna wale wasiomuomba Allah kabisa,na hawa ni wale wenye kufanya kiburi kwa kuacha kumuabudia Allah.
2- Kuna wale Wanaomuomba Allah lakini Wanaomuomba na Mungu mwingine hawa ni washirikina.
3-Kuna wale Wanaomuomba Allah peke yake na kumuabudu yeye pekee kwa kumtakasia ibada na dua hawa ni watu wa tauhidi.
Tanbih:
Hii riwaya iliyoitaja sheikh-Allah amrahamu-
الدعاء مخ العبادة
ambayo wameizoofisha baadhi ya wanawavyuoni ina maana sawa na ile riwaya inayosema.
الدعاء هو العبادة .
Kwa hiyo hapa tunapata faida kuwa dua haiwi isipokuwa ibada.
Imepitiwa na : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 27, 1443H ≈ December 2, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•