⏪ودليل الخوف قوله تعالى:
{ فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ }
Na dalili ya kuogopa ni kauli yake Allah -aliyetukuka-:
{Basi msiwaogope hao (washirikina); bali niogopeni Mimi kama mkiwa nyinyi ni waislamu (kweli)}
Aal Imran:175
Ufafanuzi unaotokana na sher’he za wanawavyuoni:
Shekh Allah amrehemu baada ya kutaja baadhi ya aina za ibada kwa ujumla, akaanza kuzitaja ibada kwa kuzichanganua kwa kuzitaja mojamoja na dalili zake.
Akaanza kutaja ibada ya hofu/kuogopa na dalili yake inayojulisha kuwa kuogopa ni ibada ambayo haifai kuipeleka kwa asiyekuwa Allah, na kuipeleka kwa asiyekuwa Allah ni ushirikina mkubwa unaomtoa mtu katika Uislamu.
Na hofu /uwoga umegawanyika sehemu tatu:
١- خوف العبادة ويسمى
(خوف السر).
1- Hofu ya ibada, na inaitwa hofu ya siri.
Nayo ni kuogopa uogopaji wa kiibada, hiyo ni hofu iliyoambatana na mapenzi na kutukuza na kujidhalilisha kwa Allah, na aina hii ya kuogopa kuipeleka kwa asiyekua Allah ni ushirikina mkubwa unaomtoa mtu katika uislamu.
Mfano : Pale Mtu atakapomuogopa asiyekua Allah katika lile ambalo hakuna anayeliweza isipokua Allah , kama vile akamuogopa mtu fulani au kitu fulani kuwa kinaweza kumtia maradhi,au kumuua au kumuua mwanaye, kama vile walivyo wengi katika wajinga ambao huwaogopa majini au wachawi au maiti na hili huwapelekea kufanya matendo mbalimbali ya kishirikina ili waepukane na hichi wanachokihofia kutoka kwao, bila shaka huu ni ushirikina mkubwa unaomtoa mtu katika duara la uislamu na kumuingiza katika ushirikina.
٢- الخوف الطبعي
2- kuogopa /hofu ya kimaumbile :
Nako ni kukiogopa kitu cha kichodhahiri ambacho kina uwezo wa kufanya kile ambacho mtu anakihofia kwake, kama vile kumuogopa nyoka, au akamuogopa adui au mnyama mkali, moto, na hofu ya aina hii ni hofu inayoruhusiwa ikiwa sababu zake zimetimia , kama alivyosema Allah -aliyetukuka- kuhusu mtume wake Musa-amani iwe juu yake- pindi alipotoka akiwa na hofu kutokana na Firauni na watu wake akaelekea sehemu za Madiani :
{فَخَرَجَ مِنْهَا خَآئِفًا يَتَرَقَّبُ}
Basi (Musa) akatoka, hali anaogopa.
Al-qasas 21.
٣-الخوف المحرم.
3- Kuogopa/hofu iliyoharamishwa,
Nako ni Kuogopa viumbe ukaacha kutekeleza yale aliyoyaamrisha Allah au akayafanya yale ambayo yameharamishwa juu yako.
mfano Mtu akaacha kuswali kwa Kuogopa watu watamuona ,anaona akisimama kuswali watu watamtia dosari, au zikampita baadhi ya swala kwa kuhofia kuwa akienda kuswali atafukuzwa kazi, n. k.
Hukumu ya hofu hii haramu kwa sababu inampelekea mtu kuacha yale ambayo Allah ameyawajibisha juu yake au kuyafanya yale ambayo Allah ameyaharamisha, pamoja na kwamba hofu hii si katika aina za ushirikina lakini ni haramu.
Mpitiaji : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 9, 1443H ≈ Dec 12, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•