⏪ودليل الرجاء قوله تعالى:
{ فَمَن كَانَ يَرْجُواْ لِقَآءَ رَبِّهِۦ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَٰلِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِۦٓ أَحَدًۢا }
Na dalili ya kutaraji ni kauli yake Allah aliyetukuka-:
Basi mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Molawake Mlezi}
Al-kahf 110
Ufafanuzi unaotokana na sher’he za wanawavyuoni.
Sheikh -Allah amrahamu- katika kuzitaja, aina za ibada kwa kuzifafanua akataja aina ya pili ya ibada nayo ni :
الرجاء :
Kutaraji:
Na kutaraji ni katika ibada za moyo na maana ya kutaraji ni:
Kutumaini na kupenda kile kinachotarajiwa ,nako kumegawanyika sehemu mbili:
١-الرجاء الطبعي.
Matarajio ya kimaumbile/ya kawaida.
Nayo ni:
1-Kutaraji kitu kwa mtu ambaye anakimiliki hicho kitu na huku ni kutaraji kwa maumbile hakuna ubaya mfano: Ukataraji kuwa baba yako atarudi safari yake leo kwa sababa inawezekana akarudi, au ukataraji kupewa zawadi na jirani yako na mfano wa matarajio haya ya kimaumbile ambayo viumbe wanayamiliki.
٢- رجاء العبادة.
2-Kutaraji (ambako ni) ibada:
Kutaraji ambako ni ibada nako ni kutumaini kutaraji kitu ambacho hakuna anayekimiliki isipokuwa Allah mfano ukatumaini na kutaraji kuponywa maradhi, au ukataraji kuingizwa peponi au kuokolewa na moto au kukingwa na shari za majini au uchawi n.k, bila shaka haya ni matarajio ya kiibada ambayo hayatarajiwi kwa yeyote isipokuwa kwa Allah, na mwenye kuyataraji haya kutoka kwa kiumbe kama Jini,mzimu,kaburi, walii bila shaka atakuwa amemshirikisha Allah ushirikina mkubwa unaomtoa katika uislamu.
Na kutaraji alikokutaja sheikh hapa anakusudia aina hii ya matarajio ya ibada na vilevile miongoni mwa matarajio ya ibada pia ni mtu :
Kutamani na kutaraji thawabu za Allah na msamaha wake na rehma zake
Tanbih:
Tumeona katika hiyo aya kwamba yule anayetaraji kwa maana mwenye kutumaini thawabu kwa Allah na kutaraji kumuona na kukutana naye basi afanye matendo mema iwe ni sababu ya kupata yale anayoyataraji.
Na matendo mema ni yale yaliyotimiza sharti mbili:
1- Kumtakasia nia Allah katika hiyo ibada.
2- Na iwe ni ibada ambayo Mtume -swala na salam za Allah ziwe juu yake- ameifundisha yaani ibada ambayo ipo katika sheria.
Mwisho:
Kutaraji kulikokuwa kuzuri ni mtu akawa anafanya ibada na akataraji thawabu zake kutoka kwa Allah, au mtu akaleta toba na akataraji kuwa toba yake imekubaliwa, ama kutaraji bila ya matendo mema huku ni kujihadaa na Kutamani kulikokuwa kubaya na ni uwongo mfano mtu akataraji msamaha wa Allah na hali haleti toba kwa makosa aliyoyafanya, au akataraji kuingizwa peponi na hali hafanyi matendo mema ambayo ni sababu ya kuingia peponi.
Mpitiaji : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 11, 1443H ≈ Dec 15, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•