Misingi mitatu na dalili zake .Makala namba (17)

⬅️ ودليل التوكل قوله تعالى:

{‎وَعَلَى اللَّهِ فَتَوَكَّلُوا إِنْ كُنْتُمْ مُؤْمِنِين‎}🌱

Na dalili ya kutegemea ni kauli yake Allah aliyetukuka:

{Na tegemeeni juu Allah pekee ikiwa nyinyi ni wenye kuamini}.

(Surat Maidah aya ya 23)

و قوله تعالى:

{وَمَنْ يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ}🌱

(الطلاق:٣)

{ Na anayemtegemea Allah (basi) yeye Allah humtosheleza }

Ufafanuzi unaotokana na sherehe za wanavyuoni:

Kutegemea ni katika ibada kubwa ya moyo na maana yake ni :

“Ukweli wa moyo kumuelekea Allah kwa kuegemeza mambo yote kwake pamoja na kutekeleza sababu”.

Kwa hiyo ibada hii ya kutegemea inatimia pindi vitakapokusanyika vitu viwili :

1- Ni kuyaegemezesha mambo yote kwa Allah aliyetukuka na kushinda .

2- Kutoiyangalia sababu aliyoyafanya baada ya kuitekeleza.

Uchambuzi:

Muumin anajua kuwa kufanya sababu ni katika kumtegemea Allah,lakini anapoifanya sababu fulani hujua kuwa sababu peke yake haziwezi kusababisha kupata yale anayoyakusudia kuyapata bali huwenda akapata au asipate,

Kwa sababu ili mtu ayapate anayoyakusudia ni kuwepo vitu (kadha) na miongoni mwa hivyo:

1- Kutekeleza sababu ,mfano kumeza vidonge baada ya kutajiwa na tabibu huku ni kufanya sababu ya kupona kwa hiyo unapomeza kidonge hapo umetekeleza sababu .

2- Kufaa kwa sehemu ya kufanywa hiyo sababu ambayo inakusudiwa kutekelezwa : Mfano mtu anapomeza kidonge cha maradhi fulani huwenda ile dawa isifanye kazi ima kwa kukosea kipimo,au huwenda katika mwili wake kuna kitu ambacho huiharibu hii dawa au kwa sababu nyingine mbalimbali.

3- Sehemu iepukane na kile kinachoenda kinyume na hapo,mfano: ukameza vidonge vya aina mbili ambavyo havitakiwi kumezwa mara moja .

Na kubwa zaidi tena ni jambo la mwanzo : Ni Allah kuidhinisha , yaani kukadiria isaidie hiyo dawa, kwa sababu hakuna kinachotokea isipokuwa kwa kadari ya Allah .

Mfano: Mtu ameazimia safari kwa gari na akaandaa kila kitu na akaikagua gari yake polepole ,na akafanya kila sababu ya kuhakikisha kuwa anafika salama, na akaendeesha polepole .

Lakini haya aliyoyafanya si sababu ya kusalimika pekee ,bali kuna vitu ambavyo vipo katika miliki ya Allah ,kwa sababu huwenda akagongwa na gari kubwa na kumuangamiza au kuvamiwa na majambazi.

Kwa hiyo sababu pekee haikamilishi jambo ,na vile vile haitakikani kwa mja kuacha kutekeleza sababu, kwa kuwa kutekeleza sababu ni katika ukamilifu wa kumtegemea Allah, lakini haitakiwi kwa mja kuigeukia/kuiangalia sababu ,kama walivyosema maimamu wa wema waliopita:

“ Kuzingatia/kuziangalia sababu ni kuitia dosari (ibada) ya kutegemea na kuitia dosari tauhidi, na kuzifuta sababu kuwa zisiwe sababu ni kuitia dosari akili”.

Maana ya maneno haya:

Unapofanya jambo lako fulani usiitegemee sababu uliyoitekeleza kwa sababu kufanya hivyo ni upungufu wa kumtegemea Allah na upungufu wa tauhidi, na pia kuacha kuzitekeleza sababu ni kuitia dosari akili ni kama vile mtu anayeomuomba Allah amruzuku hali ya kuwa hajishughulishi na kazi yoyote na kudai kuwa anamtegemea Allah! .

Kwa hiyo lililolawajibu juu ya mja ni kukusanya vitu viwili:

1-Kumtegemea Allah

2-Kutekeleza sababu.

Faida:

Na katika aya ya kwanza tumeona kuwa Allah -aliyetukuka- ameamrisha kumtegemea yeye , na maadamu ameamrisha hilo basi hiyo ni ibada na Allah anaipenda na anairidhia.

Na pia katika aya hiyo Allah amehusisha kutegemea kwake yeye pekee.

Tanbih:

Hakuna katazo la kumuakilisha mtu katika yale ambayo mtu anaruhusiwa kumuakilisha mwengine yaani uwakala kwa maana uwakala ni jambo la kidhahiri linaloruhusiwa lakini kutegemea ni ibada ya kimoyo ambayo mwenye kuipeleka kwa asiyekuwa Allah basi ameingia katika ushirikina .

Mpitiaji : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 24, 1443H ≈ Dec 28, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *