https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
📖 ثَلَاثَةُ الْأُصُوْل وأدلتها 📖
Misingi mitatu na dalili zake .
makala namba (10):
♦فإذا قيل لك ماالأصول الثلاثة التي يجب على الإنسان معرفتها
Pindi utakapoulizwa ni ipi misingi mitatu ambayo ni lazima juu ya mwanaadamu kuijua?
1⃣ فقل معرفة العبد ربه
2⃣ ودينه
3⃣ ونبيه محمد ﷺ
1-Basi sema ni mja kumtambua mola wake
2- na kutaimbua dini yake
3- na kumtambua Mtume wake Muhammad swala na salam za Allah ziwe juu yake.
♦ فإذا قيل لك من ربك
فقل ربي الله الذي رباني وربى جميع العالمين بنعمه وهو معبودي ليس لي معبود سواه
pindi utakapoulizwa ni nani Mola wako
basi sema Mola wangu ni Allah ambaye amenilea na amevilea viumbe vyote kwa neema zake naye ndiye ninayemuabudu sina mimi ninayemuabudu asiyekua yeye.
↩والدليل قوله تعالى
( الحمد لله رب العالمين )
وكل ما سوى الله عالم وأنا واحد من ذلك العالم
na dalili ni kauli yake Allah aliyetukuka
{“Sifa njema zote ni za Allah Mlezi wa kila kiumbe”}
na kila kisichokua Allah ni kiumbe na mimi ni mmojawapo katika hao viumbe.
Maelezo ya muandaaji:
Shekh -Allah amrehemu- baada ya kubainisha misingi mitatu kwa ujumla akaanza kuibainisha mmoja baada ya mwengine kwa dalili zake .
Na itambulike kuwa haya maswali matatu mja ataulizwa kaburini
na makusudio ya sheikh imamu Muhammad bin Abdil-Wahhab – Allah amrahamu – kutunga kitabu hiki na akakiita ” Misingi mitatu ” ni kuelezea misingi hii mitatu .
Na yule atakaye yafahamu masuala haya na akayafanyia kazi basi atapewa taufiki ya kujibu maswali haya kaburini,
Ama yule ambaye hutamka maneno haya bila ya kujua makusudio yake kama vile mwenye kutamka tamko la kumpwekesha Allah, lakini akawa hana yakini na kile anachokitamka au mwenye kutamka kwa kuiga au kwa ada, bila ya kuingia katika moyo wake na wengi watakao shindwa kujibu maswali haya kaburini ni mfano wa watu hawa.
Tanbihi:
Muislamu lazima ayafahamu masuala ya itikadi kwa dalili na ayaamini na kuyaitakidi, na linalowajibika hapa ni kujua dalili ya masuala haya ya itikadi kama haya ya maswali ya kaburini japo mara moja katika umri na akaamini na kuitakidi kile kilichojulishwa na dalili na akidumu na hali hii mpaka kufa kwake basi huyo ni muumini aliyekufa katika imani na wala si sharti kwa mtu awe amehifadhi dalili yake na namna ya kutoa dalili lakini wajibu ni kujua na kuitakidi japo mara moja katika umri wake na kudumu na itikadi hiyo mpaka kifo.
Na pia: Maana ya swala :Nani Mola wako Mlezi? mja atapoulizwa kaburini ni:
Nani Muabudiwa wako?.
kwa maana makusudio hapa ni kuulizwa ni nani uliyekuwa akimuabudia duniani na hili ndilo kusudio la kuletwa Mitume ni kuwalingania watu wampwekeshe Allah katika ibada.
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa Dhul-Qaadad 9, 1442H ≈ June 19, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•