MISINGI MITATU NA DALILI ZAKE .(Makala no.11)

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

📖 ثلاثة الأصول وأدلتها

Misingi mitatu na dalili zake .

Makala namba ( 11)

♦فإذا قيل لك بما عرفت ربك

◾ فقل بآياته
◾ ومخلوقاته
▫ومن آياته الليل والنهار والشمس والقمر ▫ومن مخلوقاته السموات السبع والأرضون السبع ومن فيهن وما بينهما

pindi utakapoulizwa kwa kitu gani umemtambua Mola wako mlezi ?

Basi sema : (Nimemtambua) kwa alama zake,na viumbe vyake,na miongoni mwa alama zake ni usiku na mchana na jua na mwezi,

na miongoni mwa viumbe vyake ni Mbingu saba na Ardhi saba na vilivyomo ndani yake na vilivyomo baina yake .

↩والدليل قوله تعالى:

وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ .

Na dalili (ya hilo) ni kauli yake Allah -aliyetukuka-:

{Na miongoni mwa ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi .Basi msilisujudie jua wala mwezi , msujudieni Allah ambaye ameviumba hivyo ikiwa nyinyi mnamuabudu yeye tu }

فُصِّلت : ٣٧.

Maelezo na ufafanuzi unaotokana sherehe za wanachuoni :

Katika kipengele hiki sheikh -Allah amrahamu- anataja dalili za msingi wa kwanza ambao ni kuamini kuwa Allah ndiye Mola mlezi anaye walea viumbe wote na muumba wa hivyo viumbe .

Shekh akaanza kutaja dalili zinazothibitisha uungu wake na ulezi wake na lengo ni kuwa baada ya kuyajua haya viumbe watajua kuwa hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa yeye aliyeviumba hivi viumbe.

Na hapa sheikh -Allah amrahamu- ametenganisha baina ya alama na viumbe pamoja na kua katika Qur-an kuna aya zinazothibitisha kuwa Mbingu na Ardhi ni katika ishara /alama , lakini sheikh ametenganisha kwa sababu ishara /alama vinajulisha zaidi makusudio kwa anayeulizwa kwa sababu usiku na mchana ni viumbe ambavyo hudhihiri na kuondoka ,na pia jua na mwezi , yaani huwa vinabadilika kama tunavyoona usiku na mchana na jua na mwezi, ama mbingu na ardhi muda wote huviona kwa ajili hii ndiyo maana sheikh akatenganisha .
Na huu ni ufupi wa ufafanuzi wa sheikh Swaleh Aalu- Sheikh -Allah amuhifadhi-

Na alama na ishara zinazoonesha kuwepo kwa Allah mmoja anayestahiki kuabudiwa ni aina mbili :

1-Za kiulimwengu

2- Na za kisheria.

Alama za kiulimwengu ni viumbe vyote tunavyoviona na tusivyoviona , na alama na ishara za kisheria ni wahyi yaani vitabu vyake alivyowateremshia mitume wake kwa maana ni maneno yake na hizi alama si viumbe kwa sababu maneno ya Allah si kiumbe.

Na kuna baadhi ya wanachuoni wanazigawa hizi alama za kiulimwengu katika vigawanyo vitatu:

1- Alama za juu kama : Mbingu ,Jua ,mwezi,sayari,nyota n.k

2- Alama za ardhini kama :Ardhi na vilivyomo ndani yake kama bahari mito n.k

3- Alama za kinafsi : Yaani mwanadamu mwenyewe akiingalia nafsi yake ni alama tosha ya kuwepo kwa Allah mmoja anayestahiki kuabudiwa .

Mazingatio:

Miongoni mwa hivyo viumbe na alama zinazoonesha kuwepo kwa Allah ni usiku na mchana na vyote hivi vinajulisha ukamilifu wa uwezo wake na ukamilifu wa hikma zake na ukamilifu wa huruma yake mfano kuna faida mbalimbali ambazo watu huzipata kutokana na mabadiliko ya usiku na mchana mfano : katika wakati wa mchana viumbe hufanya shughuli zao , na wakati wa usiku hupumzisha miili yao .

Jua pia hutembea katika mpangilio aliouweka Allah haliendi kinyume na mpangilio aliyoupangilia Allah na viumbe wanapata faida mbalimbali na manufaa mengi sana kutokana na jua kama vile:

Kutengemaa kwa maisha ya watu, na kwa wanyama ,na mimea , pia tunapata joto ,tunapata mwangaza ambao unatufanya tusihitajie taa wakati wa mchana n.k .

Vilevile mwezi ambao Allah ameuwekea vituo 28 kila usiku una kituo chake na mwezi huanza mdogo kisha hukua kidogo kidogo mpaka ukakamilika kisha huanza kupungua kama vile mwanadamu anavyozaliwa akawa kitoto kichanga kisha hukua mpaka akawa mzee na akaanza kupungua tena akarudi mwanzo na akawa kama alivyozaliwa na akawa dhaifu na mnyonge , na bila shaka katika hilo kuna alama tosha na ishara ya kuwepo Allah anayestahiki kuabudiwa pekee .

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 12, 1442H ≈ June 22, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *