قال الشيخ/ سليمان الرحيلي وفقه الله:
Amesema sheikh Suleiman Arruhailiy -Allah amuafikishe :
إن الغالب على من يريد الدنيا أن يكون ذليلا، ولا يمكن أن ترى العزة في عبد يريد الدنيا،
Bila shaka aghlabu yule anayeitaka dunia huwa ni dhalili na wala haiwezekani ukaona utukufu kwa mja anayeitaka dunia,
بل هو يتذلل للعبيد الأغنياء من أجل الدنيا، ويكذب من أجل طلب الدنيا،
Bali yeye hujidhalilisha kwa waja (wa Allah) matajiri kwa ajili ya dunia na hudanganya kwa ajili ya kuitafuta dunia ,
ويبيع دينه وكرامته بعَرَضٍ من الدنيا! فكان كالعابد لها؛ لأنه متذلل من أجلها.
na huuza dini yake na utukufu wake kwa vitu vya dunia ,basi (mtu huyo) huwa ni kama mwenye kuiabudia dunia kwa sababu yeye ni mwenye kujidhalilisha kwa ajili ya hiyo (dunia) .
📚 إرشاد المريد ٢٩٩/٢
Maelezo ya mfasiri:
Mtu ambaye lengo lake ni kuipata dunia na mapambo yake bila shaka huwa dhalili kwa sababu ya kuitafuta dunia na yupo tayari kujidhalilisha kwa matajiri , kuuza dini yake na utukufu wake, kudanganya kwa ajili ya dunia na kwa ajili hii mtu huyu anazingatiwa kana kwamba ni mwenye kuiabudia dunia kwa kule kujidhalilisha kwake kwa ajili ya kuitafuta dunia na kuiweka kwake moyoni ,na mtu huyu Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-amemuombea dua ya kuangamia pale aliposema :
تَعِسَ عبدُ الدِّينَارِ، وَعَبْدُ الدِّرْهَمِ، وَعَبْدُ الخَمِيصَةِ،
Aangamie yule mwenye kuiabudia dinar ,na yule mwenye kuiabudia dirham ,na mwenye kuyaabudia mavazi,
إنْ أُعْطِيَ رَضِيَ، وإنْ لَمْ يُعْطَ سَخِطَ، تَعِسَ وَانْتَكَسَ، وإذَا شِيكَ فلا انْتَقَشَ،
Kama akipewa (anachokihitaji) huridhia na kama hakupewa hukasirika, aangamie na aanguke kifudifudi na anapochomwa na miba asiwe na uwezo wa kuitoa …
رواه البخاري ومسلم
Maana ya hadith:
Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-anatutahadharisha tusiwe ni watwana na watumwa wa matamanio yetu kwa kuitanguliza dunia katika kutafuta pesa,mavazi na mengineyo katika vitu vya dunia na tukaacha kuyatanguliza ya akhera ambayo ni yenye kubaki, na mtu huyu mwenye kuitanguliza dunia kama vile kutafuta pesa ,n.k
Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- amemuombea dua ya kuangamia kwa sababu mtu huyu pindi anapopewa kile anachokikusudia humridhia Allah ,na kama hakupewa hukasirika ,kwa ajili hii akaombewa dua ya kuangamia na udhalili na kama itatokea atapatwa na shida basi asipatikane wa kumsaidia .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 7, 1444H ≈ Nov 1, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•