أختي في الله مباركة،
Dada yangu kwa ajili ya Allah umebarikiwa,
لقدوم شهر رمضان،
Kwa kuingia mwezi wa Ramadhani,
ومبارك لك في الحمل،
Na ubarikiwe katika ujauzito (wako),
واسألي الله أن يجعله مخلوقًا سويًّا،
Na muombe Allah amfanye (huyo mtoto) kuwa ni kiumbe aliyekuwa sawa,
سليمًا معافًا،
Aliyesalimika (na) aliyekuwa na afya,
ويهون عليك في حملك وولادتك،
Na (Allah) akuwepesishie ujauzito wako na kujifungua kwako,
وإليك بعض النَّصائح:
Na chukua baadhi ya hizi nasaha:
1 – إذا كنت في الشُّهور الثَّلاثة الأولى من الحمل،
☞ 1- Ukiwa katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito,
وهي مرحلة تخلُّق الجنين،
Na hiyo ni hatua ya kuumbwa mtoto,
فبإمكانك الصَّوم بسهولةٍ ويسرٍ،
Basi inawezekana kwako kufunga kwa sahali na wepesi,
إذا لم يكن هناك أيّ مضاعفاتٍ،
Kukiwa hakuna nyongeza yoyote (ya mashaka),
وليس للصَّوم أيُّ تأثيرٍ على الحمل،
Na funga haina athari yoyote juu ya ujauzito,
عند الإفطار عليك باختيار الطَّعام المتنوع الغنيّ،
Wakati wa kufuturu jilazimishe kuteua vyakula tofauti tofauti vilivyojitosheleza,
بكلِّ عناصر الغذاء،
Kwa aina zote za vyakula vya msingi,
من بروتيناتٍ،
Ambavyo ni protin,
وكربوهيدراتٍ،
Na kabohaidreti (wanga),
وفيتاميناتٍ،
Na vitamin,
ودهونٍ،
Na mafuta,
فقد ثبت أنَّ هذه العناصر تساعد بفضل الله على تكوين جنين متعافي،
Na bila shaka imethibiti (kitabibu) kuwa hivi (vyakula) vya msingi husaidia kwa fadhila za Allah kujengeka kitoto chenye afya,
أمَّا إذا كنت كثيرة القيء والوحم،
Ama ukiwa ni mwingi wa kutapika na (kuwa) na hamu kubwa ya kula baadhi ya vyakula,
فهذه الأعراض لها عاملٌ نفسيٌّ كبيرٌ،
Basi viashiria hivi sababu kubwa inayopelekea ni (sababu ya) kinafsi,
والوضع يعتمد على حالتك،
Na mazingira (ya kufunga)yanategemea hali yako,
فكثرة القيء تؤدِّي إلى ارتفاعِ نسبة الأسيتون في البول،
Basi wingi wa kutapika hupelekea kunyanyuka (kuzidi) asilimia ya acetone katika mkojo,
وخللٍ في نسبة الأملاح،
Na mvurugiko katika kiwango cha chumvi,
والتَّمثيل الغذائي،
Na mfumo wa mmeng’enyo wa chakula,
وهذه الحالات تحتاج علاج بالمستشفي،
Na hali hizi zinahitaji kutibiwa hospital,
وعليه فلا ننصح بالصَّوم.
Na juu ya hilo basi hatutoi nasaha kufunga (mtu huyu),
أمَّا الحالات البسيطة من القيء (مرَّةً أو مرَّتان) باليوم،
Ama hali chache za kutapika (mara moja au mbili) kwa siku,
فتوكلي على الله،
Basi mtegemee Allah,
واسأليه العون على الصِّيام،
Na muombe Allah msaada juu ya funga,
بعد أخذ حليب كافي وقت السُّحور.
Baada ya kupata maziwa fresh yakutosha wakati wa daku.
🔍 الدكتورة / سميرة العوضي، استشاري أمراض النساء والولادة.
Daktar Samirah Al-‘iwadhiy, Mtoa ushauri wa maradhi ya wanawake na uzazi.
الطبعة الثانية (1429 ھ- 2008)، طبعت بدعم من شركة باب الخير.
[ (Makala ya) Chapa ya pili (2008 – 1429H), imechapwa kwa msaada kutoka shirika la mlango wa heri ].
Maelezo ya mfasiri :
Makala hii katika toleo hili jipya aliipitia ndugu yangu katika imani daktar Abubakar Mubaraka Mhagama-Allah amuhifadhi – na akaongezea ufafanuzi ufuatao:
Kama mja mzito atafunga katika hali hiyo iliyotajwa basi akithirishe pia kunywa maji usiku, na mfano wa vyakula ambavyo anatakiwa ale ni hivi :
1- Vyakula vya wanga kama vile : Ugali, viazi vitamu,viazi vikuu, ndizi za kupika n.k.
2-Vyakula vya vitamini :Matunda, mboga za majani.
3- Vyakula vya mafuta :Karanga, nazi, pia maziwa yana mafuta n.k.
Vyakula vyenye protini :Nyama ya ng’ombe, mbuzi,kondoo,kuku,samaki, n.k
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde
Asshafiy .
Imehakikiwa na daktari :
Abubakar Mubaraka Mhagama
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imerudiwa: Shabani 25, 1443H ≈ Mar 28, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•