Mjamzito ndani ya mwezi wa Ramadhani

Makala namba (2)

2 – في الشُّهور الوسطى من الحمل (الرابع والخامس والسَّادس)

☞ 2 – Na katika miezi ya katikati ya ujauzito (mwezi wa) wanne na watano na wasita)

ففي هذه الفترة يثقل الرَّحم،

Na katika kipindi hiki kifuko cha uzazi huwa kizito,

ويزداد ضخُّ الدَّم إليه،

Na damu huzidi kumiminika ndani yake,

لزيادة حجمه،

Kwa sababu ya kuzidi umbile lake (kifuko cha uzazi),

وكبر الجنين والمشيمة،

Na (kwa sababu ya) ukubwa wa mtoto na kifuko cha kumuhifadhi mtoto,

ومن الظَّواهر الفسيولوجيَّة الملموسة انخفاض ضغط الدَّم،

Na katika mambo yanayodhihiri katika viungo vya mwili vinavyohisiwa ni presha ya damu kushuka,

وهذا ما يسبب الشُّعور بالدّوخة،

Na (hali) hii husababisha kuhisi kizunguzungu,

وأحيانًا الإغماء بعد الوقوف طويلًا،

Na mara nyingine (hata) kuzimia baada ya kusimama muda mrefu,

في هذه الحالات ينصح بأخذ كميات كبيرة من السَّوائل،

Na muda huu anashauriwa kupata (kunywa) kiwango kikubwa cha vimiminika (vinywaji),

خصوصًا في فصل الصَّيف،

Haswa katika kipindi cha joto,

وتجنب الإجهاد،

Na kujiepusha na kujichosha,

وينصح بتعجيل الإفطار على سوائلَ دافئةٍ بعد التَّمر،

Na anapewa nasaha (ushauri) wa kuharakisha kufuturu kwa vimiminika (vinywaji) vya uvuguvugu baada ya (kula) tende,

وتأخير السُّحور كما أمرنا رسولنا – عليه الصَّلاة والسَّلام –

Na kuchelewesha kula daku kama alivyotuamrisha mtume wetu – Swala na salamu za Allah zimfikie –

فقال:

Akasema:

{ لا يزال النَّاس بخيرٍ ما عجلوا الفطر }

{ Watu wataendelea kuwa na heri maadamu wanaharakisha kufuturu }

📚 متفقٌ عليه.

[ Wameafikiana Al-bukhaariy na Muslim ]

🔍 الدكتورة / سميرة العوضي، استشاري أمراض النساء والولادة.

Daktar Samirah Al-‘iwadhiy, Mtoa ushauri wa maradhi ya wanawake na uzazi.

الطبعة الثانية (1429 ھ- 2008)، طبعت بدعم من شركة باب الخير.

Ufupi wa maelezo:

Mama mjamzito katika miezi hii mitatu yaani mwezi wa nne, wa tano na wa sita, kama atafunga anatakiwa akithirishe kunywa vinjwaji vingi baada ya kufuturu haswa katika kipindi cha kiangazi na pia aache kufanya kazi zitakazo mchosha na pia anashauriwa awahishe kufuturu kwa maana jua likizama tu na pia baada ya kumaliza kufuturu na tende anywe vinywaji vuguvugu na pia acheleweshe kula daku .

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Imehakikiwa na daktari: Abuu Raiyaan Alo Issa Kabwe

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Shabani 27, 1443H ≈ Mar 30, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *