قَالَ اللَّهُ -تَعَالَى- :-
Amesema Allah -aliyetukuka-:
«يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌ وَلَا بَنُونَ ، إِلَّا مَنْ أَتَى اللَّهَ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ»
“Siku ambayo hazitonufaisha mali wala watoto” .
“Isipokuwa yule aliyemjia Allah na moyo safi”
( الشُعَرَاء/الآيَة: ٨٨-٨٩).
قَالَ ابن القيم رَحِمَهُ اللَّهُ:-
Amesema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu-:
“وَمِنْ عَلَامَاتِ صِحَّةِ القَلْبِ:
◀ أَنْ لَا يفتر عَنْ ذِكْرِ رَبِّهِ، وَلَا يَسْأَم مِنْ عِبَادَتِهِ وَطَاعَتِهِ،
Miongoni mwa alama za uzima wa moyo :
Kutochoka kumtaja Mola wake Mlezi na kutochoka kumuabudia na kumtii.
◀ وَلَا يأنس بِغَيْرِهِ، إِلاَّ بِمَنْ يَدُلُّهُ عَلَيْهِ، وَيُذَكِّرُهُ بِهِ، وَيُذَاكِرُهُ بِهَذَا الأَمْرِ.
Kutoliwazika na mwingine isiyekuwa (Allah) isipokuwa (huliwazika) na yule ambaye anamjulisha hilo (jambo la kumtaja Allah) na humkumbusha na kumtajia jambo hili ,
◀ وأَنَّهُ إِذَا فَاتَهُ وِرْدُهُ، وَجَدَ لِفَوَاتِهِ أَلَماً أَعْظَم مِنْ تَأَلُّمِ الحَرِيْصِ بِفَوَاتِ مَالِهِ وَفَقْدِهِ،
Utakapompita uradi wake huhisi maumivu makubwa zaidi ya (maumivu) ya mwenye pupa (ya mali) kwa kuondoka mali zake na kuzikosa
◀ وأَنَّهُ يَشْتَاقُ إِلَى عِبَادَةِ اللَّهِ وَطَاعَتِهِ، كَمَا يَشْتَاقُ الجَائِعُ إِلَى الطَعَامِ وَالشَرَابِ،
Huwa na shauku ya kumuabuda Allah na kumtii kama mwenye njaa anavyokuwa na shauku ya chakula na kinywaji,
◀ وأَنْ يَكُوْنَ هَمّهُ وَاحِداً، وَأَنْ يَكُوْنَ فِيْ اللَّهِ،
Na huwa makusudio yake ni mamoja ,huwa ni kwa ajili ya Allah,
◀ وأَنَّهُ إِذَا دَخَلَ فِيْ الصَلَاةِ ذَهَبَ عَنْهُ هَمّهُ وَغَمّهُ بِالدُنْيَا، وَاشْتَدَّ عَلَيْهِ خُرُوْجهُ مِنْهَا، وَوَجَدَ فِيْهَا رَاحَتَهُ وَنَعِيْمَهُ وَقُرَّةَ عَيْنِهِ وَسُرُوْر قَلْبِهِ،
Na kwamba (moyo huo) unapoingia katika swala huondoka majonzi yake na msongo wake wa mawazo kwa sababu ya dunia ,na huwa ni uzito kwake kutoka katika hiyo (swala) ,na hupata ndani yake raha zake na neema zake na kiburudisho cha macho yake na furaha ya moyo wake,
◀ وأَنْ يَكُوْنَ أَشَحّ بِوَقْتِهِ أَنْ يَذْهَبَ ضَائِعًا مِنْ أَشَدِّ النَاسِ شُحّاً بِمَالِهِ”.
Na huwa mbakhili wa wakati wake kwenda mtupu/bila ya faida kuliko mtu ambaye ni bahili mno kwa mali zake
📚| إِغَاثَةُ الَّلهْفَان مِنْ مَكَائِدِ الشَيْطَان (ج:١ص: ٧٢).
Maelezo ya mfasiri:
Hizi ni miongoni mwa sifa za moyo mzima ulioepukana na maradhi ya utata na matamanio na huo moyo ndiyo moyo msafi ulioepukana na husuda ,chuki,bughudha ,mafundo kwa waislamu wenzake, na huu ndiyo moyo utakao salimika siku ya kiama, na miongoni mwa sifa zake ni hizi alizozitaja sheikh -Allah amrahamu-:
1- Hauchoki kumtaja Allah na kumuabudu .
2- Hapati maliwazo isipokuwa kwa kumtaja Allah au kwa kuwa na wale wanaomkumbusha kumtaja Allah .
3- Anapopitwa na uradi wake aliojiwekea kama vile kuhitimisha juzu moja la quran kila siku huwa hana raha hujisikia vibaya mno kuliko mtu mwenye mapenzi ya mali aliyepoteza mali zake .
4- Huwa na shauku kubwa ya kumuabuda Allah kama vile mwenye njaa anavyokuwa na shauku ya chakula.
5- Siku zote makusudio yake ni kupata radhi za Allah .
6- Anapoingia katika ibada ya swala husahau shida zake zote za dunia na hutamani hiyo swala isimalizike kwa raha anayoipata na namna anavyoburudika.
7- Hapotezi muda katika yale yasiyomnufaisha kwa maana ni bakhili mno wa muda wake zaidi ya mtu ambaye ni bakhili wa mali zake ! .
Bila shaka kwa sababu ya uzito wa jambo hili ndiyo maana miongoni mwa dua za mtume- swala na salamu za Allah ziwe juu yake ilikuwa ni hii :
”وَأَسْأَلُكَ قَلْباً سَلِيْماً، وَلِسَاناً صَادِقاً“.
“Na nakuomba moyo uliosalimika na ulimi ulio mkweli” .
سِلْسِلَةُ الأَحَادِيْث الصَحِيْحَة لِلْأَلْبَانِي رَحِمَهُ اللَّهُ تَعَالَى، رَقْمُ الحَدِيْث (٣٢٢٨).
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 21, 1443H ≈ Jan 24, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•