للشيخ العلامة عبد العزيز ابن باز – رحمه الله
(Fatwa ya) mwanachuoni mkubwa Abdullah ibn Baaz- Allah amrahamu-
الرسالة رقم – (٤٢)
Ujumbe namba arobaini na mbili,
بيان كيفية تغسيل من توفي وهو جنب،
Kubainisha namna ya kumuosha yule aliekufa hali ya kuwa ana janaba,
السؤال :
Swal: 🎙
إذا توفي الإنسان وعليه غسل،
Atakapokufa mtu na hali ana wajibika kuoga josho la wajibu,
هل غسل الجنازة يكفي عن ذلك الغسل
Je kuoshwa kwake josho la kifo litamtosheleza na kutooshwa na hilo josho (la janaba)?
الجواب:
Jawabu: 📚
الغاسل إذا كان يعلم ينويهما جميعا،
Muoshaji atakapokuwa anajua atanuia (majosho) yote mawili,
وإذا كان لا يعلم سده غسل الميت،
Na atakapokuwa hajui (basi hilo janaba) litatoshelezwa na josho la maiti,
📚 المصدر: فتاوى نور على الدرب (ج١٣ ص ٤٥٢)
Maelezo ya mpitiaji:
Mtu atakapofariki na hali anajosho la wajibu kama hedhi, nifasi, janaba, haiwajibiki kuoshwa mara mbili bali akioshwa mara moja tu yaani akioshwa josho la kifo litakuwa, limetosheleza hilo josho jingine la wajibu,kwa sababu zikikusanyika kwa mtu sababu mbili zinazowajibisha kuoga akioga josho moja litatosheleza majosho yote mawili.
قال النووي رحمه الله في “المجموع” (١٢٣/٥) :
Amesema Annawawiy-Allah amrahamu- katika “Al-majmu’u” (5/123):
” مذهبنا أن الجنب والحائض إذا ماتا غسلا غسلا واحدا ,
Madhehebu yetu (ya kishafii) kwamba mwenye (josho la) janaba na hedhi pindi watakapofariki wataoshwa josho moja,
وبه قال العلماء كافة إلا الحسن البصري فقال: يغسلان غسلين. قال ابن المنذر: لم يقل به غيره “
na hivi (hivi) wamesema wanavyuoni wote isipokuwa Al-hasan Al-baswry ,(yeye) amesema: wataoshwa majosho mawili .
(Na) amesema ibn Al-mundhir : Hakusema (kauli hii) yeyote (isipokuwa yeye).
Mpitiaji : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Toleo la pili : Mfungo nane 6, 1443H ≈ Dec 10, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•