السؤال:
Swali: 🎤
ما حكم قولهم:
Ni ipi hukumu ya kauli yao (kwa maiti):
” يا أيتها النفس المطمئنة؟ “
” Ewe nafsi iliyotulizana?”
الجواب:
هذا غلط، وما يدريهم فذلك؟
Jawabu: 📚
Hili ni kosa,
Na lipi linowajulisha hilo (walilozungumza),
بل المشروع الدعاء له بالمغفرة،والرحمة ويكفي ذلك.
Bali (kinachotakiwa) kisheria ni kumuombea msamaha,na rahmah na hilo linatosha.
📚 مجموع فتاوى ابن باز
Maelezo kutoka kwa mfasiri- Allah amuhifadhi
Maana ya maneno haya ya sheikh ni kwamba: Haifai kuhukumu au kukata moja kwa moja kwa mtu mmoja maalumu kwamba ni mtu wa peponi kama vile kumwambia maneno haya: ” Ewe nafsi iliyotulizana “
ila ikithibiti kwamba huyo ni mtu wa peponi kama vile maswahaba waliobashiriwa pepo wakiwa duniani,
Na pia haifai kukata kwa mtu mmoja kwamba ni wa motoni ila wale ambao Allah ameeleza au Mtume- swala na salamu za Allah ziwe juu yake- kama Abuu Lahab na wengine-,au vilevile mtu aliyekufa katika ukafiri pia tunahukumu kuwa ni wa motoni milele kama walivyoeleza baadhi ya wanawavyuoni.
Tunachotakiwa ni kuzungumza kwa ujumla tu kwa kusema: ” Waumini wote ni peponi.
Nukta Muhimu:
Ikiwa maiti ni muislamu wa sawa sawa yaani muumini basi tunataraji kwake kwamba ni mtu wa peponi, na akiwa ni muislamu muovu basi tunamuogopea adhabu! kwa maana huenda akaadhibiwa.
kinachotakiwa ni kukithirisha kuwaombea dua waislamu wenzetu walio tangulia kama alivyosema sheikh -Allah amrahamu-.
“Ewe Allah tusamehe sisi na ndugu zetu walio tutangulia katika imani “
Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Toleo la,pili :Mfungo nane 7, 1443H ≈Dec 11, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•