MOYO NI KAMA CHOMBO!

قال ابن القيم – رحمه الله- :

Amesema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu -:

فالخبيث يتفجر من قلبه الخبث على لسانه وجوارحه

Basi mtu mbaya hububujika kutoka moyoni mwake mabaya (yanayodhihiri) katika ulimi wake na viungo vyake

والطيب يتفجر من قلبه الطيب على لسانه وجوارحه

Na mtu mzuri hububujika kutoka moyoni mwake mazuri (yanayodhihiri) katika ulimi wake na viungo vyake

📚زاد المعاد ١ /٦٨

Maelezo ya mfasiri:

Amesema kweli ibn l-Qayyim -Allah amrahamu- na waarabu pia wanasema hivi:

كُلُّ إِنَاءٍ بِمَا فِيْهِ يَنْضَحُ

Kila chombo hutiririka (humwagika) kile kilichomo ndani yake .

Maana ya msemo huu :

Mwanadamu ni kama chombo kama unavyoona chombo kilichojazwa maziwa kinapomiminwa humwagika maziwa na hakiwezi kumwagika maji basi ni hivihivi mwanadamu ambaye moyo wake umejaa tabia njema kama ukarimu , unyenyekevu n.k ,tabia hizi hudhihiri katika maneno yake na mwenendo wake, na vilevile mtu mwenye tabia mbaya kama vile: husuda ,chuki kiburi na kupekua makosa ya watu, vilevile tabia hizi hudhihiri katika kinywa chake na viungo vyake na hata kama akijitahidi kuzificha ni lazima zitadhihiri kama alivyosema Zuhair ibn Abbi Sulmaa :

وَمَهما تَكُن عِندَ اِمرِئٍ مِن خَليقَةٍ

وَإِن خالَها تَخفى عَلى الناسِ تُعلَمِ

Na tabia yoyote itakayokuwa kwa mtu, hata kama akidhania (kuwa tabia) hiyo inafichikana kwa watu (basi) itajulikana tu

Mwisho:

Tunamuomba Allah azipambe nyoyo zetu na tabia njema

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 6, 1445H ≈ Oct /9, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *