MOYO WA MWANADAMU HUZUNGUKA SEHEMU HIZI !

قال ابن القيم – رحمه الله : –

Amesema Ibnul Qayyim – Allah amrahamu :

للقلب ستة مواطن يجول فيها

Moyo una sehemu sita unazozizunguka

لا سابع لها :

(Na) wala hauna (sehemu) ya saba :

ثلاثة سافلة،

(Sehemu) tatu ni za chini ( za udhalili) ,

وثلاثة عالية،

Na (sehemu nyingine) tatu ni za juu (tukufu) ,

فالثلاثة السافلة:

Basi (sehemu) tatu za chini (za udhalili) ni :

( ١) دنيا تزين له،

(1) Dunia inayojipamba kwa ajili yake (inayomvutia),

(٢) ونفس تحدثه،

(2) Na nafsi inayomsimulia,

(٣) وعدو يوسوس له،

(3) Na adui anayemtia wasiwasi,

والثلاثة العالية:

Na (sehemu) tatu (ambazo) ni za juu (tukufu) ni :

(١) علم يتبين له،

(1) Elimu inayombainikia ,

(٢) وعقل يرشده،

(2) Na akili inayomuongoza,

(٣) وإله يعبده.

(3) Na muabudiwa anayemuabudu.

📚 الفوائد لابن القيم (ص ٩٩)

Maelezo ya mfasiri :

Haya ni maeneo sita ambayo moyo wa mwanadamu huyazunguka ,na hakuna eneo la saba bali ni haya sita tu ,na katika maeneo haya sita maeneo matatu ni maeneo duni na ya udhalili ambayo mtu mpumbavu hushughulishwa nayo nayo ni :

1-Mtu kushughulika na dunia tu kama vile kukusanya mali na mapambo mbalimbali bila shaka mwenye kufanya hivi huyu nafsi imeporomoka na kudhalilika .

2- Kushughulika na nafsi kwa mambo yasiyokuwa na faida akhera kama vile kushughulika na kula ,kuvaa,kunywa na kuacha ya akhera yake .

3- Shetani anayemtia wasiwasi kwa sababu ya kushughulika kwake na dunia na kuistarehesha nafsi yake basi Shetani humshawishi kupita njia hii.

Ama maeneo matatu ambayo yapo juu yaani ni matukufu ,na yule aliyeafikishwa na Allah hutilia umuhimu haya :

4- Kusoma elimu ya kisheria na kutilia umuhimu hilo na kusoma dini ni alama ya kutakiwa kheri na Allah kama alivyosema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-:

” مَنْ يُرِدِ اللَّهُ بِهِ خَيْرًا يُفَقِّهْهُ فِي الدِّينِ “

“Yule ambaye Allah humtakia kheri humpa ufahamu katika dini ”

5- Kuitumia akili yake katika mambo ya kheri ,na akili humuongoza mwanadamu.

6- Kumuelekea Allah kwa kumuabudia peke yake.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 22, 1443H ≈ Aug 20, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *