Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
الرَّافِضِيُّ عَلِيّ جُمْعة مَيُوْنغ – عَلَيْهِ مِنَ اللّٰهِ مَا يَسْتَحِقُّ- يُحاولُ أنْ يَنَالَ مِنَ الصَّحَابِيِّ الْجَلِيْلِ عُثْمَانَ بْنِ عَفَّان
MSHIA ALIY JUMA MAYUNGA- ALLAH AMLIPE MABAYA ANAYOSTAHIKI- AKIJARIBU KUMTUKANA SWAHABA MTUKUFU UTHMAN BIN AFFAN -ALLAH AMRIDHIE-
قال في في ترجمته للقرآن إلى اللغة السواحلية:
AMESEMA KATIKA TARJAMA YAKE YA QURAN KWA LUGHA YA KISWAHILI:
Uthman bin Affan,ndiye mtu wa kwanza kufunga milango ya Haki,na yeye ndiye wa kwanza kufungua milango ya dhulma.
Marejeo: QUR’AN INAYOBAINISHA
Tarjama na Tafsir, Kiarabu na Kiswahili, Ukurasa wa 508 tafsir ya suuratut taubah
Na: Ali Juma Mayunga
MAELEZO YA MWANDISHI:✍
Huyu ndio Aliy Mayunga ambaye ni mshia mkubwa hapa Tanzania nadhani mnaona jinsi gani matusi na uwongo unao bubujika kutoka kinywani mwake dhidi ya swahaba huyu mtukufu ambaye ni mkwe wa Mtume (swala na salamu za Allah zimfikie) kwa mabinti wake wawili kwa ajili hiyo hujulikana kwa jina la mwenye nuru mbili kwa maana alioa mabinti wawili wa mtume (swala na salamu za Allah zimfikie) yaani baada ya kufariki wa kwanza akaozeshwa wa pili, na ni mtu pekee katika historia aliyeoa mabinti wawili wa Mtume !
Na pia ni katika watu waliobashiriwa pepo hali ya kuwa wapo duniani, na ni katika watu wenye tabia ya haya mpaka malaika wanamuonea haya kama alivyoeleza Mtume (swala na salamu za Allah zimfikie) na Uthman (Allah amridhie) yeye ndiye aliyekinunua kisima cha Ruumah ambacho Mtume (swala na salamu za Allah zimfikie) alisema:
من يشتري بئر رومة فيكون دلوه فيها كدلو المسلمين.
رواه البخاري
NI NANI ATAKAE NUNUA KISIMA CHA RUUMAH NA UTAKUWA UCHOTAJI WAKE KATIKA (KISIMA) HICHO KAMA UCHOTAJI WA WAISLAMU (WENGINE).
…فله الجنة.
NA ATAPATA PEPO
رواه البخاري .
Na kusima hiki kilinunuliwa na Uthman (Allah amridhie) kwa huu ni waqfu ambao Uthman uliutoa na akabashiriwa pepo na kubwa zaidi na la maajabu HIKI KISIMA MPAKA LEO KIPO NA BADO KINALETA MANUFAA kwa hiyo thawabu bado zinamiminika tu kwa swahaba huyu mtukufu.
Haya turudi kwa Mayunga , na ukienda katika ukurasa huu wenye matusi ya Uthman (Allah amridhie) utaona juu ya matusi haya kuna maelezo tena ameandika kwa herufi kubwa na kukoleza wino:
MASWAHABA WAOVU.
Kisha tunaambiwa Mashia wa Tanzania hawawatukani Maswahaba !!!
Tunamuomba Allah kinga na upotevu
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Iliandaliwa February 7,2018M ,ikahakikiwa na kurudiwa tena Shawwal 8, 1442H ≈ May 20, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•