MSIBA MKUBWA!

قال مِسعر بن كِدام:

Amesema Mis’aru bin Kidam:

كنتُ أمشي مع سفيان الثوري، فسأله رجلٌ،

Nilikuwa nikitembea na Sufian Thauriy ,(basi) kuna mtu (alitokea) akauomba (kitu),

فلم يكن معه ما يُعطيه، فبكى،

na (Sufiani) hakuwa na cha kumpa, basi (Sufian) akalia,

فقال له: ما يبكيك؟

na (Mis ‘ar) akamuuliza (Sufian): Kipi kinachokuliza?

قَالَ: وأيُّ مصيبةٍ أعظمُ من أن يُؤمِّل فيك رجل خيرًا، فلا يصيبه عندك؟

(Sufiani) akajibu: Ni msiba upi mkubwa zaidi kuliko (wa) mtu kutaraji heri kwako , na (akawa) si mwenye kuipata kwako hiyo (heri) ?

المصدر:

 مكارم الأخلاق للخرائطي (141)

Maelezo ya mfasiri:

Anaeleza Mis’aru bin Kidam-Allah amrahamu- kuwa siku moja alikuwa akitembea na Sufian Thauriy -Allah amrahamu- ghafla akatokea mtu akamuomba msaada Sufian lakini Sufian hakuwa na chochote cha kumpa huyo mtu, basi Sufiani akawa analia kwa kule kukosa kwake cha kumsaidia huyu aliyemuomba, na akaliona jambo hilo kuwa ni msiba mzito uliompata ! kitendo cha mtu kumuomba kwa maana mtu huyo ametaraji heri kutoka kwake kisha akawa hana cha kumpa jambo hilo lilimuumiza mno mpaka likamtoa machozi ,na hii ndiyo kawaida ya watu wema, kama ilivyotokea kwa wale maswahaba ambao walishindwa kupata gharama za maandalizi ya kushiriki katika jihadi ya vita vya Tabuk na walipokuja kwa Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- naye hakuwa na vipandwa vya kuwabeba basi walikuwa wakilia kutokana na shauku yao kubwa ya kuipigania dini ya Allah kama alivyosema Allah-aliyetukuka – :

{ وَلَا عَلَى الَّذِينَ إِذَا مَا أَتَوْكَ لِتَحْمِلَهُمْ قُلْتَ لَا أَجِدُ مَا أَحْمِلُكُمْ عَلَيْهِ تَوَلَّوْا وَأَعْيُنُهُمْ تَفِيضُ مِنَ الدَّمْعِ حَزَنًا أَلَّا يَجِدُوا مَا يُنْفِقُونَ ﴾

Na wala (hapana dhambi) juu ya wale waliokujia ili uwapatie cha kupanda,(waende vitani) ,ukasema: “Sina cha kukupandisheni juu yake; wakarudi , na hali macho yao yanamiminika machozi kwa huzuni ya kukosa kupata masurufu hayo .

التوبة:92

Muandishi : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 26, 1445H ≈ Feb/7, 2023M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *