Mtiririko wa vikadi vya mafunzo ya itikadi kwa watoto ,kitabu namba mbili .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

KITABU CHA PILI :

1 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .

(Sehemu ya pili) :

س رقم: ١
Swali no.1:

لِمَاذَا يَجِبُ عَلَيْكَ أَنْ تَتَعَلَّمَ الْعَقِيْدَةَ ؟

Kwanini inawajibika juu yako kujifundisha itikadi?

ج:
Jawabu:

لِكَيْ أُرْضِيَ اللّٰهَ، وأَنْجُوَ مِنَ الْفِتَنِ ،وَمِنْ عَذَابِ اللّٰه.

Ili nimridhishe Allah na niokoke na fitina na (niokoke) na adhabu za Allah .

سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.

[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amuhifadhi]

Maelezo ya Mfasiri:

Mzazi /Mlezi hapa utamuelezea mtoto kuwa: ni wajibu juu yake kijifundisha aqidah yaani itikadi sahihi ya dini yetu ya Kiislamu ambayo wameipokea Maswahaba kutoka kwa Mtume wetu-swala na salamu za Allah zimfikie- na utamueleza kuwa kujifundisha itikadi ya wema waliopita ni wajibu kwa sababu kufanya hivyo ni kumridhisha Allah na kuridhiwa na Allah kwa sababu Allah yeye hauridhii ukafiri kwa waja wake kama alivyosema :

إِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ اللَّهَ غَنِيٌّ عَنكُمْ ۖ وَلَا يَرْضَىٰ لِعِبَادِهِ الْكُفْرَ ۖ وَإِن تَشْكُرُوا يَرْضَهُ لَكُمْ ۗ

Kama mkikufuru, basi Allah si mwenye haja nanyi; lakini haridhii ukafiri kwa waja wake; na kama mkishukuru ,Yeye huwa radhi nanyi .

الزمر ٧

Maana ya aya :

Anasema Allah katika aya hii :Kama mutamuamini Mola wenu mlezi na mukamtii atawaridhia kwa kushukuru kwenu ,na shukurani inayokusudiwa ya viumbe kwa Allah ni kumuamini kwao Allah na kumtii lakini Allah ametaja shukurani kwa maana ya kumuamini na kumtii .

Na pia kujifundisha itikadi sahihi ya kiislamu ni sababu ya kuepukana na fitna na mabalaa ya dunia na akhera.

Na pia itikadi sahihi ni sababu ya kuepukana na adhabu za Allah.

Usikose makala namba 2 inayofuata in shaa Allah

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 11 , 1444H ≈ Dec 5, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *