MUISLAMU KATIKA MAISHA YAKE YOTE YUPO KATIKA SWAUMU !

قال الإمام ابن رجب الحنبلي -رحمه الله- :

Amesema imamu ibn Rajab Al-hanbaliy -Allah amrahamu-:

الدُّنيا كلها شهر صيام المتقين وعيد فطرهم يوم لقاء ربهم

(Maisha ya) dunia yote ni mwezi wa swaumu ya wacha Mungu na sikukuu ya kufuturu kwao ni siku ya kukutana na Mola wao mlezi

ومعظم نهار الصيام قد ذهب وعيد اللقاء قد اقترب.

Na sehemu kubwa ya mchana wa funga umeondoka (imepita) na sikukuu ya kukutana na (Allah) imekaribia

وقد صمت عن لذات دهري كلها …

Na bila shaka nimejizuia na starehe (ya machafu) maisha yangu yote …

ويوم لقاكم ذاك فطر صيامي

Na siku ya kukutana na nyinyi hiyo ni siku ya kufungua funga yangu .

المصدر :

لطائف المعارف فيما لمواسم العام من الوظائف لابن رجب الحنبلي -رحمه الله-

Maelezo ya mfasiri:

Muumini anaishi katika dunia katika uhai wake wote kana kwamba yupo katika ibada ya funga kutokana na kule kujizuia kwake na machafu , na muumini huishi katika hali hii ya kuizuia nafsi yake kutokana na machafu akisubiri siku yake atakayokuja kufuturu ambayo ni siku ya idi nayo ni siku atakayokutakana na Mola wake yaani ni siku ya kufa kwake

Kwa hiyo muumini katika hii dunia yupo katika Swaumu ya kujizuia na maovu na siku yake ya eid ni siku ya kufa kwake , na pia siku za kuondoka duniani zimekaribia sehemu kubwa ya umri umeondoka na baada ya siku chache tutaondoka .

•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 1 , 1444H =Apr 20, 2023M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *