قال طلحة البغدادي :
Amesema Twal-hatu Al-baghdadiy-Allah amrahamu – :
” ركبتُ مَع الإمامِ أحمدَ فِي سفينة، فكانَ يُطيلُ السكوتَ، فإذا تَكلَّمَ قَال:
Nilipanda jahazi mimi pamoja na imamu Ahmad, basi alikuwa akinyamaza muda mrefu, na pindi anapozungumza husema :
اللَّهُمَّ أَمِتنا عَلى الإسلامِ والسُّنَّة
Ewe Allah tufishe juu ya uislamu na sunnah.
[طبقاﺕالحنابلة١/ ١٧٩]
Maelezo ya mfasiri :
Allah amrahamu imamu Ahmad ambaye ni mmoja katika maimamu wetu wanne wa madhehebu ya fiqih ya ahlu sunnah wala-jama’a, hapa tunajifundisha kuwa inatakiwa kwa kila muislamu afanye juhudi ya kuujua ule uislamu alioufundisha Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – na maswahaba wakashikamana nao, kwa maana unaweza ukawa muislamu lakini haupo katika ule uislamu alioufundisha Mtume _swala na salamu za Allah zimfikie – na hii ndiyo maana ya sunnah ambayo imamu Ahmad alikuwa akimuomba Allah aichukue roho yake hali yeye yupo katika uislamu na sunnah kwa maana yupo katika ule uislamu ambao maswahaba waliuchukua kutoka kwa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 20, 1445H ≈ Dec 4, 2023M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•