قال سفيان بن عيينة-رحمه الله-:
Amesema Sufiani bin Uyainah – Allah amrahamu – :
يُستحب للرجل إذا دعا أن يقول
في دعائه : اللهم استرنا بسترك الجميل ،
Inapendeza kwa mtu pindi atapoomba dua aseme katika dua yake:
Ewe Allah tusitiri kwa stara yako nzuri,
قال سفيان :
akasema Sufiani :
ومعنى الستر الجميل :
Na maana ya stara nzuri :
أن يستر على عبده في الدنيا ثم يستر عليه في الآخرة من غير أن يُوَبِّخَهُ عليه.
Ni kumsitiri mja wake duniani kisha akamsitiri akhera bila ya kumlaumu kwa kumuaibisha.
المجالسة وجواهر العلم ٢٨٦/١
Maelezo ya mfasiri :
Bila shaka katika fadhila za Allah juu kwa muumini kama ilivyothibiti katika hadithi kuwa Allah atamuweka karibu muumini siku ya kiama na ataweka kizuizi baina yake na watu ili wasimuone huyo mja akafedheheka mbele yao, kisha atamtajia makosa yake kwa siri na huyu mja muumini atakiri hayo makosa yake na pale atakapokuwa na yakini kuwa yeye ni mwenye kuangamia basi hapo ndipo atakapodirikiwa na msamaha wa Allah, na Allah atasema:
فإنِّي قد سَترتُهَا عليكَ في الدُّنيا،وأنا أَغفِرُهَا لكَ اليومَ
Basi bila shaka mimi nimeyasitiri hayo (madhambi) yako duniani, na leo hii nakusamehe bila ya kukufedhehesha.
رواه البخاري ومسلم.
Lakini stara hii ni haswa kwa waumini pekee ama makafiri na wanafiki wao watafedheheshwa mbele ya viumbe kama alivyosema Allah – aliyetukuka-:
وَيَقُولُ ٱلْأَشْهَٰدُ هَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ كَذَبُواْ عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ أَلَا لَعْنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلظَّٰلِمِينَ
na mashahidi watasema : “Hao ndio waliomzulia Mola wao mlezi uwongo. Sikilizeni laana ya Allah iko juu ya madhalimu.
هود ١٨
Hivi ndiyo watakavyo fedheheshwa makafiri na wanafiki siku ya kiama kwani Malaika ambao walikuwa wakiandika matendo yao waliyoyafanya duniani, watatoa ushahidi juu ya hayo, na pia mitume nao watakuwa mashahidi.
Tanbih : Maelezo haya yanatokana na hadithi iliyopokewa na Bukhariy na Muslim.
Tunamuomba Allah atusamehe madhambi yetu na kutusitiri duniani na akhera.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 22, 1445H ≈ Dec 6, 2023M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•