قال الإمام ابن القيم -رحمه الله تعالى-:
Amesema imam ibn l-Qayyim -Allah aliyetukuka amrahamu-:
• قال -ﷺ-:
Amesema-swala na salamu za Allah zimfikie-:
«سلوا الله العافية واليقين فما أعطي أحدٌ بعد اليقين شيئاً خيراً من العافية فسلوهُما الله تعالى».
Muombeni Allah afya na yakini, basi hajapatapo mtu kupewa chochote kilicho bora zaidi kuliko afya basi muombeni Allah aliyetukuka- viwili hivyo
↩️ و لا يتم صلاح العبد في الدارين إلا باليقين و العافية.
Na wala hakutimii kutengemaa! kwa mja katika nyumba mbili /duniani na akhera isipokuwa kwa yakini na afya
⏪ فاليقين يدفع عنه عقوبات الآخرة، و العافية تدفع عنه أمراض الدنيا في قلبه و بدنه.
Basi yakini itamlinda kutokana na adhabu za akhera, na afya itamlinda kutokana maradhi ya duniani katika moyo wake na mwili wake.
📚[زاد المعاد (١٩٧/٤)
Maelezo ya mtarjumu-:
Neema ya afya na kulindwa na mabalaa mbalimbali ni neema kubwa ambayo mtu hawezi kuifahamu mpaka augue kama walivyosema waliosema:
الصحة تاج على رؤوس الأصحاء لا يعرف قدرها إلا المرضى
Afya ni taji juu ya wenye afya (na) hatambui thamani yake isipokuwa mgonjwa
Ndio! ukitaka kujua neema ya afya basi tembelea hospitalini uone jinsi watu wanavyougulia maradhi mbalimbali .
Na vile vile afya ya kwanza kabisa ambayo muislamu anatakiwa aiombe ni afya ya kulindwa na kuepushwa na maradhi ya moyo ambayo ni :
1- Maradhi ya utata : ambayo humuingiza mtu katika ushirikina au katika bida’a
2- Maradhi ya matamanio: Ni nafsi kutamani yale ambayo inayatamani na kufuata matamanio na kuingia katika uharamu kama uzinifu, liwati, n, k.
Na yakini maana yake ni kuwa na imani ya kweli isiyokuwa na shaka ambayo ni sababu ya mtu kuepushwa na moto wa Jahannam
Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 23, 1443H ≈ November 28, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•