• قال تعالى :
Amesema (Allah) aliyetukuka-:
﴿ وَالبَلَدُ الطَيِّبُ يَخْرُجُ نَبَاتُهُ بِإِذْنِ رَبِّهِ ﴾
Na ardhi nzuri hutoa mimea yake (mizuri) kwa idhini ya Mola wake Mlezi.
الأعراف : ٥٨
•• قال ابن القيم رحمه الله :
Amesema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu-:
« فالمؤمن ؛ إذا سمع القرآٓن ، وعقِله ، وتدبّره ،
بان أثرَه عليـه ، فشُـبّه بالبلـد الطـيب ».
Basi muumini pindi anaposikia Quran na akaifahamu na akaizingatia hudhihiri athari yake juu yake basi (kwa ajili hii) akafananishwa na ardhi nzuri .
📚 بدائع التفسير (٤١٠/١)
Maelezo :
Wamesema wanavyuoni kuwa muumini mfano wake ni kama ardhi nzuri yenye rutuba yenye kuotesha mimea vizuri kwa idhini ya Allah, hivi ndivyo athari ya Qurani inavyodhihiri katika muonekano wa muumini.
Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 4, 1443H ≈ Jan 7, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•