MUUMINI SIKU ZOTE YUPO KATIKA NEEMA.
قال الشيخ عبد الرزاق بن عبد المحسن البدر – حفظه الله-:
Amesema sheikh Abdul-Rrazzaq bin Abdil-Muhsin Al-badr-Allah amuhifadhi-:
« … والابتلاء في هذه الحياةِ الدنيا تارة يكون بالرخاء والنعمة ، وتارة يكون بالشدة والمصيبة ، تارة يكون بالصحة وتارة يكون بالمرض ، تارة يكون بالغنى وتارة يكون بالفقر ، فالمؤمن عرضة للبلاء في هذين البابين : باب الشدة وباب الرخاء .
Kujaribiwa katika maisha haya ya dunia mara nyingine huwa kwa (kupewa) raha na neema, na mara nyingine huwa kwa shida na masaibu na mara nyingine huwa kwa afya na mara nyingine huwa kwa uzima ,mara nyingine huwa kwa utajiri na mara nyingine huwa kwa ufakiri,basi muumini ni mwenye kuyaingia mabalaa katika milango hii miwili: mlango wa shida na mlango wa raha
وهو من خيرٍ إلى خير في كل ابتلاءاته ، ولهذا ثبت في المسند من حديث أنس رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال : ((عَجَبًا لِلْمُؤْمِنِ !! لَا يَقْضِي اللَّهُ لَهُ شَيْئًا إِلَّا كَانَ خَيْرًا لَهُ ))؛
Na yeye (hutoka) katika heri na huingia katika heri katika kila mitihani yake,na kwa ajili hii imethibiti (hadithi) katika musnad katika hadithi (alizopokea) Anas -Allah amridhie-kwamba Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-amesema-:
{{Ni ajabu jambo la muumini! Allah hamkadirii chochote isipokuwa huwa ni heri kwake}}
وقوله : (( شيْئًا )) يتناول كل ابتلاء سواء كان شدة أو كان رخاء ، والمؤمن في كل ابتلاءاته من خير إلى خير ؛
Na kauli yake ((chochote)) inakusanya mitihani yote sawa sawa iwe ni ya shida au raha na muumini katika mitihani yake yote hutoka katika heri na huelekea katika heri
وذلك أن المؤمن الموفق إذا ابتلاه الله جل وعلا بالشدة والعسر ، والمرض والفقر ، ونحو ذلك من الابتلاءات تلقاها بالصبر ؛
Na hilo ni kwa kuwa muumini aliyepewa taufiki pindi Allah-aliyetukuka na aliyejuu -anapomjaribu kwa shida na ugumu na maradhi na ufakiri na mfano wa hayo katika mitihani (muumini) huipokea kwa kusubiri
فيفوز في هذا النوع من الابتلاء بثواب الصابرين ،
Basi (muumini) hufaulu katika aina hii ya majaribio kwa kupata thawabu za wenye kusubiri
وإذا ابتلاه الله جل وعلا بالرخاء واليسر ، والصحة والعافية ، والغنى والسعة ؛
Na pindi Allah-aliyeshinda na aliyejuu -anapomjaribu kwa kumpa raha na wepesi na afya uzima na utajiri na wasaa,
فإنه في هذا النوع من الابتلاء يكون شاكرا لله جل شأنه فيفوز بثواب الشاكرين…»
Basi hakika huyo (muumini) katika aina hii ya majaribio anakuwa ni mwenye kumshukuru Allah (ambaye) -limetukuka jambo lake-basi hufaulu kwa kupata thawabu za wenye kushukuru .
المصدر :
📚 مقتبس من مقال بعنوان:
الابتلاء » والمنشور في الموقع الرسمي
Maelezo ya mfasiri:
Muumini siku zote yupo katika neema pindi anapotahiniwa kwa matatizo mbalimbali na akasubiri basi yupo katika ibada kubwa ya kusubiri, na pindi anapotahiniwa kwa kukunjuliwa neema mbalimbali na akamshukuru Allah kwa neema hizo basi yupo katika heri pia.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 29, 1443H ≈ Mar 2, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•