MWENYE KUTAKA KUFUNGUKIWA NA NJIA YA UONGOFU

قال شيخ الإسلام ابن تيمية – رحمه الله –

Amesema Sheikh l-islam ibn Taimiyyah – Allah amrahamu-:

إِذَا افتَقَرَ العَبدُ إلى اللَّهِ ودَعَاهُ وأدمَنَ النَّظَرَ في كلامِ اللَّهِ وكَلامِ رَسُولِهِ ﷺ وكَلامِ الصحَابةِ والتابِعِين وأئِمَّةِ المُسلمِينَ انفَتَحَ لَهُ طَرِيقُ الهُدَى.

Pindi mja atakapomuhitajia Allah na akamuomba na akadumisha (jicho lake) kutizama maneno ya Allah na maneno ya Mtume wake – swala na salamu za Allah zimfikie – na maneno ya maswahaba na wafuasi wa maswahaba na wanachuoni wa kiislamu (basi) kutamfungukia njia ya uongofu.

مجموع الفتاوى ٥ / ١١٨

Maelezo:

Jambo la kwanza: Muislamu anatakiwa amuelekee Allah – aliyetukuka – na adhihirishe haja zake kwake, kama alivyokuwa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – akifungua swala zake za usiku kwa kuomba dua hii:

اللَّهمَّ ربَّ جبريلَ وميكائيلَ وإسرافيلَ فاطرَ السَّمواتِ والأرضِ عالِمَ الغيبِ والشَّهادةِ أنتَ تحكُمُ بينَ عبادِكَ فيما كانوا فيهِ يختلِفونَ اهدِني لما اختُلِفَ فيهِ منَ الحقِّ بإذنِكَ إنَّكَ تهدي من تشاءُ إلى صِراطٍ مستقيمٍ.

Ewe Allah Mola mlezi wa Jibril na Mikail na Israfil (ewe) muumba wa mbingu na ardhi mjuzi wa yaliyojificha na yanayodhihiri wewe unahukumu baina ya waja wako katika yale ambayo walikuwa wakitofautiana ndani yake, niongoze katika haki na usawa katika hizi tofauti, hakika wewe unamuongoza unayemtaka kwa kumuelekeza njia iliyonyooka na ya sawa.

روام مسلم ٧٧٠

Ufafanuzi:

Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – alikuwa akimuomba Allah amthibitishe na ampe taufiki ya kushikamana na njia iliyonyooka bila shaka asiyekuwa yeye anatakiwa azidishe.

Jambo la pili: Ni kudumu na kukithirisha kuyasoma maneno ya Allah (Qur’ani), kwa sababu ndani yake kuna uongofu kama alivyosema Allah:

{هُدًى لِلْمُتَّقِينَ}

{ Ni uongofu kwa wacha Mungu }

Jambo la tatu: Ni kudumu na kukithirisha kusoma hadithi za Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – kwa sababu mwenendo wake ni uongofu.

La nne na la tano: Ni kusoma historia na mwenendo ya Maswahaba na wale walioishi na maswahaba na maswahaba ndio walioishi na Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – na kuupokea uislamu kutoka katika kinywa chake na hauwezi kuufahamu uislamu mpaka upitie kwao na pia wale waliosoma na kupokea mafundisho kutoka kwa hao maswahaba.

La sita: Ni kusoma historia na maisha ya wanachuoni na maimamu wa dini hii kama vile maimamu wa madhehebu manne ya Ahlu sunnah wal-jamah na katika wanachuoni wetu wa zama hizi mwenye kusoma historia ya Sheikh ibn Baz, ibn ‘Uthaimin, Al-albaaniy – Allah awarahamu wanachuoni wote wa kiislamu – atapata faida kubwa na atajua njia yao katika kulingania na manhaji (njia) waliyokuwa nayo katika kulingania.

Haya ndio mambo ambayo mtu akiyafanya basi atafungukiwa na njia ya uongofu kwa idhini ya Allah kama alivyosema ibn Taimiyyah – Allah amrahamu.

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 28, 1443H ≈ Jan 2, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *