Mwenye kutaka kupendeza

https://www.fawaidusalafiya.net

MWENYE KUTAKA KUPENDEZA!

قَالَ ابنُ القَيِّم – رَحِمَهُ اللَّـهُ –

Amesema ibn l-Qayyim – Allah amrahamu-:

الجَمَالُ البَاطِن يُزيِّنُ الصُّورَة الظَّاهِرة، وإنْ لَم تَكُن ذَات جَمَال..، فإنَّك تَرَى الرَّجُل الصَّالِح المُحسِن ذَا الأخلاقِ الجَميلةِ مِن أحْلَى النّاس صُورَة، وَإِن كانَ أَسود أو غيْر جَميل، وَلا سِيَما إِذا رُزِق حظا من صَلاةِ اللَّيلِ، فَإنَّها تُنوِّر الوَجه وَتُحسِّنُه.»

Uzuri wa ndani (moyo) huupamba muonekano wa nje, hata kama (muonekano) si wenye uzuri, basi bila shaka wewe unamuona mtu mwema mwenye tabia njema ni katika watu wenye muonekano mzuri, hata kama akiwa mweusi au si mzuri na haswa akiruzukiwa fungu katika swala ya usiku basi bila shaka huko (kuswali usiku) huutia nuru uso na kuupamba.

رَوضَةُ المُحبِّين (٣٢٠/١)

Maelezo: Uzuri wa moyo kuwa na ikhlaswi katika matendo yaani kufanya matendo kwa ajili ya Allah – aliyetukuka – kumuabudu Allah kwa ibada za moyo kama kuogopa, kutegemea, kutaraji n.k, na kujipinda katika ibada ya kisimamo cha usiku haya yote ni sababu ya mtu kuvutia na kupendeza katika macho ya waumini.

بعض السلف: من كثرت صلاته بالليل حسن وجهه بالنهار.

Wamesema baadhi ya wema waliopita: Mwenye kukithirisha swala zake usiku uso wake hunawiri (wakati wa) mchana.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

Telegram: https://t.me/fawaidussalafiyatz Imechapishwa: February 10, 2021M, Jumaadal -aakhir 28, 1442H.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge nasi Telegram upate faida nyingi zilizokupita, Kujiunga bonyeza hapa: ⬇️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *