NAMNA YA KUIHAKIKI TAUHID

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

كيفـية تحقيـق التوحيـد

JINSI YA KUIHAKIKI TAUHIDI

لِلشَـّيْخ العلّامـة صـالِح بنُ فَـوْزَان الفَـوْزَان حَفِظَهُ الله

(Jawabu) la sheikh mwanachuoni mkubwa Swaalih Fauzan Al-fauzan (Allah amuhifadhi​)

السُّــــؤَال ُ:-

SWALI:- 🎙

كـيف يعـرف المسـلم أنه حقَّـق التـوحيد، ومـا الفضـل فـي تحقيـق الـتوحيد ؟

Ni vipi atatambua muislamu kuwa yeye ameihakiki tauhid na ni upi ubora (uliopo) katika kuihakiki tauhid ?

الجَـــــوَابُ:-

JAWABU:-📚

•• المسـلم لا يزكـي نفـسه ، ولا يمـدح  نفـسه ويقـول حـققتُ التـوحيد ،

Muislamu haitakasi nafsi yake na wala haisifu nafsi yake kwa kusema:

Mimi nimeihakiki tauhidi

•• وتحقـيق التوحـيد هـو : « تصـفيته مـن النـقائص ، ومـن الشـرك ، ومـن الذنـوب والمـعاصي » ، هـذا تحقيـق التوحيـد

Na kuihakiki tauhidi ni : kuitakasa kutokana na mapungufu, na kutokana na ushirikina na kutokana na madhambi na maasi na hii (ndiyo maana) ya kuihakiki tauhidi.

•• فـي فـرق بيـن المـوحِّد ومـحقق التوحيـد ، مـحقِّق التوحـيد أرفـع مـنزلة مـن المـوحِّد فقـط .

Kuna tofauti kati ya mtu wa tauhid (tu) na (yule) aliyeisafisha tauhid (huyu) aliyeisafisha tauhid ni mwenye daraja la juu zaidi kuliko mtu wa tauhid tu (asiyeitakasa)

📚 مــــن هنـــــا :-

(Marejeo yanapatikana) kutoka hapa:- ⇣⇣

https://t.co/CDeanb5HIE

Maelezo ya mtarjumu:

Kuihakiki tauhidi maana yake ni tauhidi kukita na kuthibiti katika nafsi mpaka tauhidi ikaingia sawa sawa katika moyo wa mtu na akalazimiana nayo, na mtu hawezi kulifikia daraja hili mpaka asalimike na yale yanayopingana na msingi wa tauhidi au ukamilifu wake, na vinavyopingana na tauhidi vinarudi katika asili tatu:

1- Ushirikina

2- Bida’a/uzushi

3- Maasi /maovu.

Ushirikina unapingana na tauhidi kwa ujumla .

Na bidaa inapingana na ukamilifu wake wa wajibu (wa tauhidi), na makusudio ya bidaa hapa ile isiyofikia katika daraja la ushirikina au ukafiri .

Na maasi yanatia dosari katika (tauhidi) na kupunguza thawabu zake .

Na makusudio ya kujiepusha na maasi ni kuzidisha kuwa na pupa mno katika kujiepusha na hayo maasi , na kutubu kwa haraka pindi mtu anapofanya maasi ama yule asiyetubu kwa madhambi aliyoyafanya basi hilo linatia dosari tauhidi.

Na kuihakiki tauhidi kuna daraja mbili:

1- Darasa la wajibu – nalo ni kuepukana na hayo matatu yaliyotajwa hapo juu.

2- Daraja la pili ni daraja la suna – nalo limekusanywa na (maana hii) :

Ni moyo kujaa (mapenzi) ya kumuelekea Allah na kujitupa mbele yake na kuvua kila utumwa katika moyo kusibakie ndani yake ila kumpenda Allah na kumyenyekea .

Tanbih: Maelezo haya yanatokana na maneno ya sheikh Swaleh Al-‘Uswaim -Allah amuhifadhi-

Mtarjumu : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 5, 1443H ≈ November 10, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *