https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
NAMNA YA
KUMSHUKURU ALLAH NA NAMNA KUWASHUKURU WAZAZI WAWILI
▪️قال تعالىٰ :
{ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ }
Amesema Allah aliyetukuka:
{Ya kwamba unishukuru Mimi na Wazazi wako; kwangu mimi tu ndio marejeo }
(لقمان ١٤ )
قال سفيان بن عيينة رحمه الله:
مَنْ صلَّى الصلوات الخمس فقد شَكرَ الله تعالى،
ومَنْ دَعَا لِوالدَيه في أدبار الصَّلوات فقد شَكرَهُما.
Amesema Sufiyani bin U’yaynah Allah amrehemu :
Atakayeswali swala tano hakika amemshukuru Allah -aliyetukuka -na atakayewaombea wazazi wake wawili baada ya kila swala tano basi bila shaka amewashukuru (wazazi wake).
📗( تفسير القرطبي – ٦٥/١٤ )
Maelezo ya muandaaji:
Katika aya hii Allah -aliyetukuka- anamuamrisha mwanadamu kwanza amshukuru yeye Allah -aliyetukuka- kwa kumuabudia yeye pekee na kumtakasia ibada na kutii maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake , kisha awashukuru wazazi wake kwa kuwafanyia wema na kuwalisha,kuwasikiliza na kuwatii katika mema ,kuwatembelea na kuwanyenyekea n.k , na katika wema ni kuwaombea dua haswa baada ya kufariki kama wazazi wako ni waislamu basi jitahidi kuwaombea dua kama alivyosema Sufian bin ‘Uyainah -Allah amrahamu- katika kuwashukuru wazazi ni kuwaombea dua kila baada ya kumaliza kuswali swala ya faradhi ,kwa kifupi usiache kuwaombea dua wazazi wako wawili katika maeneo mbalimbali ambayo tumehimizwa kuomba dua .
Pia katika aya hii kuna kitisho na tahadhari kama alivyosema sheikh ibn ‘Uthaimin- Allah amrahamu- kwa yule aliyeenda kinyume na amri hii pale Allah aliposema :
{Kwangu mimi pekee ndiyo marejeo} .
Maana yake :Utarejea kwangu na nitayahesabu matendo yako ,
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 9, 1442H ≈ June 19, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•