Namna ya kuswalia jeneza (maiti) [ No. 05 ]

https://www.fawaidusalafiya.net

سلسلة أحكام الجنائز.

MLOLONGO (MFULULIZO) WA HUKUMU ZA MAITI (NO. 36)

☞ NAMNA YA KUSWALIA JENEZA (MAITI)

Makala namba 05:

Au unaweza ukamuombea maiti dua nyingine iliyothibiti kama hii:

Dua namba 02:

{ اللَّهمَّ إنَّ فُلانَ بنَ فُلانٍ في ذمَّتِكَ وحَبلِ جِوارِكَ فقِهِ مِن فتنةِ القبرِ وعذابِ النَّارِ وأنتَ أهلُ الوفاءِ والحقِّ اللَّهمَّ فاغفِر لَه وارحَمهُ إنَّكَ أنتَ الغفورُ الرَّحيمُ }

{ Ewe Allah bila shaka fulani mtoto wa fulani (utamtaja jina) yupo katika hifadhi yako na yupo katika amani yako basi mkinge kutokana na mtihani wa kaburini na adhabu ya moto na wewe ni mwenye kutekeleza (ahadi) na haki, ewe Allah msamehe (makosa yake) na mrehemu bila shaka wewe ni mwingi wa msamaha na mwingi wa huruma }

Maelezo:

Swala ya maiti ni dua kwa maiti, ni juu ya muislamu ajitahidi kumuombea ndugu yake muislamu msamaha na rehema, kama dua hii ambayo imethibiti kutoka kwa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – ndani yake kuna kumuombea maiti aepushwe na mitihani ya kaburini kama vile kuulizwa maswali, giza lake, kubana, na aepushwe na adhabu ya moto. Na mwisho akamalizia kwa kusema kuwa Allah ni mwenye kutekeleza ahadi na havunji ahadi yake ya kutomuadhibu yule aliyefariki hali ya kuwa anamuabudu Allah pekee yaani mwenye kumpwekesha Allah. Na akafunga dua yake kwa kumuombea maiti msamaha wa madhambi yake na pia amrehemu kwa kulinyanyua daraja lake huko peponi.

Dua za kumuombea maiti zimekuja nyingi ila tutosheke na hizo mbili (dua namba 01 na 02). Na unaweza kusoma dua nyingineyo yoyote katika zile zilizokuja.

Tutaendelea in shaa Allah, usikose makala namba 06.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net

Imeandaliwa: Tarehe 20 – Rabi’ul – aakhir ≈ 05 – December – 2020M.

Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

JIUNGE NASI TELEGRAM UPATE FAIDA NYINGI ZILIZOKUPITA. BONYEZA HAPA KUJIUNGA: ⤵️ https://t.me/fawaidussalafiyatz •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *