Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
▪️سؤال: حدث لي أني اغتب جماعة من الأصدقاء، وندمت كثيرا على هذا العمل، وأنا الآن لا أستطيع أن أذهب إليهم في المجلس .
Swali:
Ilinitokea mimi kuwasengenya wengi miongoni mwa marafiki zangu,na nimejuta sana juu ya kitendo hiki,na mimi sasa hivi siwezi kwenda katika sehemu yao wanayoketi ,
. فهل لي توبه أو عمل أستطيع أن أعمله لأكف عن فعل ذلك؟
Basi je mimi nina toba au tendo ambalo naweza nikalifanya ili nijizuie na kuyafanya hayo (ya kusengenya)?
▪️جواب العلامة ابن عثيمين رحمه الله:
Jawabu la mwanachuoni mkubwa ibn ‘Uthaimin- Allah amrahamu-:
توبتك أن تحلهم، وتخبرهم بما قلته عنهم، وتطلب منهم أن يحلوك،
وهذا هو الذي يعتبر دواء تاما
Toba yako ni kuwataka wakusamehe,na kuwaambia yale uliyoyasema kuhusu wao,na kuwataka wakusamehe,
na hii ndiyo ambayo inazingatiwa kuwa ni dawa iliyotimia,
فإذا لم يمكن، وتخشى أن يزيد الشر بينك وبينهم،
basi kama hilo halikuwezekana,na ukaogopa kuzidisha shari baina yako na wao,
فلا بد أن تحضر المجالس التي اغتبهم فيها، وتمدحهم بما فيهم، بدون غلو ولا زيادة .
Basi hakuna budi uhudhurie vikao ambavyo umewasengenya ndani yake,na uwasifu kwa yale (mazuri)waliyokua nayo bila ya kuchupa mipaka wala kuzidisha.
📚 فتاوى على الطريق ص٧١٤.
Maelezo ya mpitiaji:
Hii ni kauli ya baadhi ya wanachuoni kwamba katika sharti za toba ya dhambi ya kusengenya ni kwenda kumuomba yule uliyemsengenya kwamba akusamehe/yaishe ,na kuna wengine wanasema inatosha kuleta toba na kumtaja vizuri katika yale maeneo uliyomsengenya ,lakini hata wale waliosema kuwa ni lazima umuombe msamaha yule uliyemsengenya pindi kutakapokuwa hakuna madhara katika hilo kama alivyosema sheikh -Allah amrahamu- hapa juu , na vilevile anasema ibn Hajar Al-Haitamiy Asshafiy- Allah amrahamu-:
“وطريق التوبة بالنسبة لمَن اغتاب المسلمين هو أن يتحلله ويطلب منه العفو
Na njia ya kutubu kwa yule aliyewasengenya waislamu ni kumuomba (yule aliyemsengenya) yaishe na kumuomba msamaha,
- إذا أمن الفتنة – أما إذا كان يُسبِّبُ الشحناء أو يسبب منكرًا آخر أو فتنة،
pindi kutapoaminika kuwa hakutotokea fitna ,ama likiwa (hilo) litasababisha ugomvi au litasababisha uovu mwingine au fitna
فإن المغتاب يذكره بالخير الذي فيه في المجالس التي ذكره فيها بسوء،
basi msengenyaji (anatakiwa) amtaje (yule aliyemsengenya) kwa heri alizokuwa nazo katika vikao ambavyo alimtaja kwa ubaya
ويرد عنه الغِيبة بجهده وطاقته، فتكون تلك بتلك إن شاء الله، مع مراعاة شروط التوبة،
na amtetee asisengenywe (tena) kwa juhudi zake na uwezo wake basi yote hayo yafanywe -Allah akitaka- pamoja na kuchunga sharti za toba (zilizobakia)
وبالله التوفيق”.
(Na yote haya) kwa taufiki ya Allah .
تطهير العيبة من دنس الغيبة (ص: ٦٢).
Tanbih:
Sharti za toba zilizobakia ni hizi :
1- Msengenyi ajivue haraka na huko kusengenya na aache kumsengenya huyo ndugu yake.
2- Ujute juu ya hilo kosa alilolifanya .
3- Aweke maazimio ya kutorudia tena
Mpitiaji Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 23, 1443H ≈ November 3, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•