قال الشيخ سليمان الرحيلي -حفظه الله تعالى -:
Amesema sheikh Suleiman Arruhailiy -Allah aliyetukuka amuhifadhi-:
لا تكون محسنًا لوالديك إلا بهذه الأمور الخمسة
Hautokuwa ni mwenye kuwafanyia wema wazazi wako ila kwa haya mambo matano
▪️الإحسان إلى الوالدين يكون :
Kuwafanyia wema wazazi wawili Kuna kuwa (hivi) :
١- ببذل المعروف :
1- kuwatendea wema
قال تعالى :
Amesema (Allah) aliyetukuka:
” وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا “
“ Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yoyote isipokuwa yeye tu. Na wazazi wawili (wafanyieni) wema ” .
٢ – وكف الأذى :
2- Na kujizui kuwaudhi:
قال تعالى :
Amesema (Allah) aliyetukuka:
” إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا “
Kama mmoja wao akifikia uzee,naye yuko kwako,au wote wawili,basi usiwaambie hata Ah! Wala usiwakemee.
٣ – وإدخال السرور :
3- Na kuingiza furaha (katika nyoyo zao) :
قال تعالى :
Amesema (Allah) aliyetukuka:
” وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا “
“ Na sema nao kwa msemo wa hishima ”
٤ – والتواضع لهما :
4-Kuwanyenyekea :
قال تعالى :
Amesema (Allah) aliyetukuka-:
” وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ “
“ Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma ” .
٥- الدعاء لهما :
5- Kuwaombea dua :
قال تعالى :
Amesema (Allah) aliyetukuka:
” وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا “
“Na usema :Mola wangu Mlezi ! warehemu hao (wazazi wangu ) kama walivyonilea utotoni”
📚الدرس الثالث من شرح كتاب التوحيد
للشيخ سليمان الرحيلي حفظه الله
Maelezo ya mfasiri:
Haya mambo matano kama haujayafanya kwa wazazi wako basi ujue kuwa bado hujawatendea wema!, hebu tuangalie wema waliopita jinsi walivyojua daraja la kuwatendea wema wazazi .
عن ابن عون:
Kutoka kwa Ibn ‘Aun:
« أن محمدا كان إذا كان عند أمه لو رآه رجل ظن أن به مرضا من خفض كلامه عندها »
“ Kwamba alikuwa Muhammad (bin Siiriin) pindi anapokuwa kwa mama yake lau mtu akimuona atadhani kwamba ana maradhi kutokana na kupunguza kwake sauti mbele yake (mama yake) ”
📚 المحاسن والمساوئ، لإبراهيم البيهقي(ص ٦١٤)
📚 حلية الأولياء (٢٧٣/٢)
Ufafanuzi wa maneno haya :
Kuongea kwa sauti ya juu mbele ya mzazi wako ni katika tabia mbaya, na katika athari hii tunapata faida jinsi gani wema waliopita walijua daraja la wazazi wawili!
Haswa mama mpaka mtu akawa anapokuwa mbele ya mama yake huwa kama mgonjwa!
Yaani ni unyenyekevu wa hali ya juu na utulivu mkubwa mbele yake!
Je, wale ambao huwatembelea wazazi wao lakini hujisikia vibaya kuketi nao na huwa hawana furaha pindi wanapokuwa nao pamoja !?
Bila shaka hawa ni waasi yaani huku ni kuwaasi wazazi.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 10, 1444H ≈ Nov 4, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•