قال العلامة ابن عثيمين – رحمه الله:
Amesema mwanachuoni mkubwa Ibn ‘Uthaimin – Allah amrahamu:
وينبغي لمن تزوج ألا يقصد قضاء الشهوة فقط،
Inatakikana kwa anayeoa asikusudie kukidhi matamanio tu,
كما هو مراد أكثر الناس اليوم،
Kama (yalivyokuwa) makusudio ya watu wengi zaidi leo,
إنما ينبغي له أن يقصد بهذا التالي:
Hakika si vinginevyo anatakiwa akusudie kwa hii (ndoa) yafuatayo:
1 – أولا:
1- Kwanza:
امتثال أمر النبي ـ عليه الصلاة والسلام ـ
Kutekeleza amri ya Mtume – juu yake swala na salamu:
« يا معشر الشباب من استطاع منكم الباءة فليتزوج »
“ Enyi kongamano la vijana mwenye kuweza gharama za ndoa basi aoe ”
٢ – ثانيا:
2 – La pili:
تكثير نسل الأمة،
Kuongeza kizazi cha umma (waislamu),
لأن تكثير نسل الأمة من الأمور المحبوبة إلى النبي ـ عليه الصلاة والسلام ـ
Kwa sababu kuongeza kizazi cha umma (wa kiislamu) ni miongoni mwa mambo yanayopendeza kwa mtume – swala na salamu za Allah zimfikie –
ولأن تكثير نسل الأمة سبب لقوتها وعزتها،
Na kwa sababu kuongeza kizazi cha umma ni sababu ya nguvu yake na kushinda kwake
ولهذا قال شعيب ـ عليه الصلاة والسلام ـ لقومه:
Na kwa ajili hii alisema (Mtume) Shu’aib – juu yake swala na salamu – kuwaambia watu wake:
وَٱذْكُرُوٓاْ إِذْ كُنتُمْ قَلِيلًا فَكَثَّرَكُمْ ۖ
{ Na kumbukeni pindi mlipokuwa wachache na (Allah) akakukithirisheni }
الأعراف: ٨٦
Araaf: 86
وامتن الله به على بني إسرائيل في قوله:
Na Allah aliwasimbulia (aliwatajia neema zake) wana wa israil kwa hili (la wingi wao) katika kauli yake:
{ وَجَعَلْنَٰكُمْ أَكْثَرَ نَفِيرًا }
{ Na tukakujaalieni ni kundi kubwa }
الإسراء: ٦
Israa:6
٣ – ثالثا:
3 – La tatu:
تحصين فرجه وفرج زوجته،
Kuhifadhi utupu wake na utupu wa mkewe,
وغض بصره وبصر زوجته،
Na kuinamisha macho yake na macho ya mkewe,
ثم يأتي بعد ذلك قضاء الشهوة.
Kisha linakuja baada ya hayo kukidhi matamanio.
الشرح الممتع ( ١٢/ ٩ – ١٠)
Maelezo Kutoka kwa Mfasiri – Allah amuhifadhi
Kwa hiyo makusudio ya ndoa Sheikh ameyapangilia kama ifuatavyo:
1- Kutekeleza amri ya Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie –
2 – Kuukithirisha umma wa kiislamu na hili halitimiii ila kwa kuzaliana kwa wingi na kuacha dhana potovu ya uzazi wa mpango wa kutokuzaa sana kwa hofu ya maisha!
3 – Kuuhifadhi utupu kutokana na machafu ya uzinifu na kumuhifadhi mkeo pia na uchafu huu na kujiepusha na kutizama haramu wewe na mkeo.
4 – kukidhi matamanio ambayo ni maumbile ya mwanadamu, lakini watu wengi wanapotaka kuoa hili la kukidhi matamanio ambalo ni lengo la nne hulifanya kuwa ni la kwanza!
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tano 6, 1443H ≈ Sep 2, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•