https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
نصيحة لمن أراد الزواج بأكثر من واحدة
NASAHA KWA MWENYE KUTAKA KUOA (MKE) ZAIDI YA MMOJA
Makala namba (1) :
1-
Kwanza kabisa jiandae kinafsi na yaweke maneno haya ya Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- mbele ya macho yako :
{ مَنْ كَانتْ لَهُ امْرَأتَانِ فَمَالَ إِلَى إحْدَاهُمَا جَاءَ يَوْمَ القيامةِ وشِقُّهُ مائلٌ }
{Yeyote mwenye kuwa na wake wawili (na zaidi) ,na akaegemea kwa mmoja wao atakuja siku ya kiama na hali moja ya bega lake limeegemea (upande mmoja) }
رواه أبو داود ٢١٣٣ ،واللفظ له، والترمذي ١١٤١ ،وغيرهما .
Maelezo:
Ni wajibu kwa mume kufanya uadilifu baina ya wakeze katika kuwalisha na kuwavesha na katika zamu , na yeyote atakayeegemea upande mmoja katika hayo basi atakuja siku ya kiama na hali ya kuwa bega lake moja limeegemea upande mmoja atakuja katika hali hii ni malipo mfano wa kila alichokifanya , kwa sababu ya kutofanya kwake uadilifu baina ya wakeze katika duniani ,kwa maana atafedheheshwa mbele ya viumbe .
2- Maandalizi yaliyokamilika kutekeleza haki za kila mmoja katika hao wake yale ambayo ni wajibu juu ya mume :Kuwalisha ,kuwavesha ,makazi n.k .
3- Zamu /kulala kwa kila mmoja .
Tanbih:
Ama mapenzi ya moyo haya mwanadamu hawezi kuyamiliki na kuyagawa sawa sawa,kama anavyosimulia mama Aisha -Allah amridhie – pale aliposema :
“كان رسولُ اللهِ عليه السَّلامُ يَقْسِمُ فيَعدِلُ، ويَقولُ: “اللَّهمَّ هذا قَسْمي فيما أملِكُ، فلا تَلُمْني فيما تَملِكُ ولا أَملِكُ”
” Alikuwa Mtume wa Allah- amani iwe juu yake-akigawa zamu na akifanya uadilifu ,na husema :
Ewe Allah !hiki ni kigao changu katika yale ninayoyamiliki ,basi usinilaumu katika yale unayoyamiliki wewe na wala (mimi) siyamiliki ”
رواه أبو داود (٢١٣٥) واللفظ له وغيره .
Maana ya hadith : Mtume -swala na salamu alikuwa akifanya uadilifu katika mambo yote ya maisha kisha humwambia Allah -aliyetukuka- kuwa yeye ameyafanya yale ambayo yapo chini ya uwezo wake ,ama yale yaliyopo katika moyo yaani moyo wake ukampenda zaidi katika moja ya wakeze hili halipo katika miliki yake .kama alivyosema Allah :
{فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ}
Kwa hiyo msielekee (upande mmoja) kabisa kabisa .
النساء: ١٣٩
Maana yake :Musikusudie kufanya ubaya bali jilazimisheni kufanya sawa katika zamu ,na huduma ya chakula kwa sababu haya ni katika
yale yanayowezekana .
4- Ajue kuwa wanawake wana wivu mkubwa haswa baina ya wake wenza na hawakusalimika na hili hata wake wa mitume -Amani iwe juu yao- ,anasema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu – :
– فإن سارة امرأة الخليل صلى الله عليه وسلم غارت من هاجر وابنها أشد الغيرة فإنها كانت جارية فلما ولدت إسماعيل وأحبه أبوه اشتدت غيرة سارة فأمر الله سبحانه أن يبعد عنها هاجر وابنها ويسكنها في أرض مكة لتبرد عن سارة حرارة الغيرة وهذا من رحمته تعالى ورأفته”
“Bila shaka Sarah mke wa (Ibrahimu) Mwandani (wa Allah)- swala na salamu za Allah zimfikie-alimuonea wivu Haajar na mwanaye (Ismail) wivu mkubwa ,kwa sababu huyo (Haajar) alikuwa ni kijakazi ,na pindi alipomzaa Ismail na baba yake (Ibrahimu) akampenda (huyo mtoto) wivu wa Sarah ulizidi ,basi Allah-utakasifu ni wake- akamuamrisha (Ibrahimu) amtenge mbali Haajar mwanaye na (Sarah) na awapeleke wakaishi katika ardhi ya Makkah ili lipate kupoa joto la wivu wa Sarah ,na huu ni katika huruma wa Allah- aliyetukuka- na upole wake ”
(زاد المعاد).
Uchanganuzi:
Hata ukirudi katika maisha ya Mtume wetu- swala na salamu za Allah zimfikie- utalikuta hili ,utaona namna mama Aisha – Allah amridhie- alivyokuwa na wivu mpaka akafikia kuvunja vyombo vya mke mwenzake ! ,lakini Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie-:alijua namna ya kuamiliana nao ,kwa hiyo mume anatakiwa alijue hili .
5- Uwezo wa kuwasimamia wanawake :
Nakusudia kuwa mtu ambaye hana uwezo wa kumsimamia mke mmoja bila shaka huyu asiongeze mke na ndio maana kuna baadhi ya nchi hapo kale zilikuwa hazimpi uongozi mtu mpaka zimchunguze je ana uwezo wa kumsimamia mkewe ?!.
6- Kujua tabia na maumbile ya wanawake kama alivyoeleza Mtume- swala na salamu zimfikie-:
إنَّ المَرْأَةَ خُلِقَتْ مِن ضِلَعٍ لَنْ تَسْتَقِيمَ لكَ علَى طَرِيقَةٍ، فَإِنِ اسْتَمْتَعْتَ بهَا اسْتَمْتَعْتَ بهَا وَبِهَا عِوَجٌ، وإنْ ذَهَبْتَ تُقِيمُهَا، كَسَرْتَهَا وَكَسْرُهَا طَلَاقُهَا.
Bila shaka mwanamke ameumbwa kutokana na ubavu uliopinda, hatokunyookea (akawa) sawa sawa, basi kama utastarehe naye utastarehe naye na hali ya kuwa ana sehemu aliyopinda ,na kama utataka kumnyoosha utamvunja na kumvunja kwake ni kumuacha .
رواه مسلم :
الصفحة أو الرقم: ١٤٦٨.
Hivi ndivyo wanawake walivyo utamuona amenyooka sawa sawa katika dini lakini ana mapungufu katika mengine , mume atambue hili asije akaongeza mke kisha akawakosa wote !au akamuacha mmoja akarudi tena katika hali yake ileile !, kutokana na kutowajua maumbile yao
Itaendelea – inshaallah .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 8, 1442H ≈ June 18, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•