NASAHA KWA MUME

الزوجة لا تستغني عن التدليل بتقدم عمرها ،أو بإنجابها طفل أو أكثر،

Mke hatosheki na kudekezwa kwa kuongezeka umri wake au kwa kuzaa kwake mtoto (mmoja) au zaidi ya mmoja

هي تبقى كوردة يحييها الاهتمام والحنان ويقتلها الإهمال والذبول ..

Yeye hubakia kama vile ua (ambalo) huhuishwa na (kule) kutunzwa na mapenzi na humua (kile kitendo cha ) kupuuzwa na kunyauka..

اهتم بها دللها لا تحرمها من حنانك وعطفك فالمرأة لا تحتاج سوى الاهتمام والكلمة اللطيفة منك،

Mjali huyo (mkeo) ,mdekeze wala usimnyime mapenzi yako na huruma wako kwa sababu mwanamke haitajii isipokuwa kujaliwa na maneno mazuri kutoka kwako

لا تنس أنك كل شيء بالنسبة لها لأخ والأب والحبيب والزوج .

Usisahau kuwa wewe ni kila kitu kwake (wewe kwake) ni kaka na baba na mpenzi na mume .

المصدر : مجموعة نصائح للزوجين

Maelezo ya mfasiri:

Ndoa ni safari ndefu sana ambayo ndani yake kuna mitihani mbalimbali na misukosuko ,na wapo baadhi ya wanaume hupunguza mapenzi kwa wake zao baada ya hao wake zao kuzaa watoto kadhaa,hapo utawaona hawana tena yale mapenzi motomoto waliyokuwa nayo kabla ya wake zao kuzaa! , na hili ni kosa kwa sababu mke anapenda kudekezwa hata kama amekuwa mtu mzima au amezaa watoto ,na wanaume wengi hawafahamu kuwa mke ni kama au zuri lenye kupendeza ambalo linahitajia kutunzwa kwa kumwagiwa maji mara kwa mara ili liendelee kuwa hai na kama litaachwa na kupuuzwa basi litanyauka na kukauka na matokeo yake kufa kabisa !

Mwisho tunawaambia wanaume watunzeni wake zenu na kuwajali,na muwatilie umuhimu na muwadekeze na kuwafanyia huruma kwa sababu hawa wanawake wanahitajia sana mambo haya na kupewa maneno matamu na musisahau kuwa nyinyi baada ya kuwaoa hao wanawake na kuwaleta katika majumba yenu mmekuwa na nafasi za kaka zao na baba zao na pia nyinyi ndiyo vipenzi kwao na waume zao .

Tanbih:

Makusudio ya kumdekeza mke ni kumdekeza kwa kumfanyia yale ambayo sheria haikuyakataza , na pia mke anatakiwa amtii mumewe katika yale yasiyokatazwa na sheria kwa sababu huo ni miongoni mwa misingi ya ndoa .

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 20, 1445H ≈ Sep /23, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *