قال شيخنا إبراهيم المحيميد حفظه الله:
Amesema sheikh wetu Ibrahimu Al-Muhaimid -Allah amuhifadhi-:
نصيحة للزوجة: تقصير الزوج لك أو ظلم الزوج لك في حقك فهو عصى الله فيك فلا تعصي الله فيه
Nasaha kwa mke:
Mapungufu ya mume kwako au dhulma ya mume katika haki zako (tambua kuwa) huyo mume amemuasi Allah kwa (kukudhulumu) haki yako,basi na wewe usimuasi Allah kwa (kutomtimizia haki zake) huyo (mumeo)
نصيحة للزوج: تغاض عما تستطيع ولاتدقق في كل صغيرة وكبيرة، وكذلك الزوجة تتغاضى عن كل شيء يزعجها لأنه يعود عليها صحيا وبدنيا
Nasaha kwa mume :
Fumbia macho kwa kuyaacha kuyafanya yale unayoweza kuyafanya (katika kumuadabisha) na wala usifuatilie kila dogo na kubwa na pia mke akifumbie macho kila kitu kinachomkera kwa sababu hilo (manufaa) yatarudi kwake kiafya na kimwili
ولنا في رسول الله ﷺ أسوة حسنة
Na sisi tuna kiigizo chema kwa Mtume wa Allah -swala na salamu za Allah zimfikie-
كذلك: لن يبق معك أحد يرعاك مثل زوجتك في أواخر عمرك لا ابنك و لا ابنتك مهما أحسنوا إليك
Vilevile (mume tambua) hakuna yeyote atakayebaki akikuchunga/kukutunza mfano wa mkeo katika kipindi cha mwisho wa umri wako, si mwanao wa kiume wala binti yako vyovyote watakavyokufanyia wema
لأنك أحسنت لزوجتك في حال قوتك وسطوة شبابك فأحسنت إليك في كبرك.
Kwa sababu wewe umemfanyia wema mkeo katika kipindi cha nguvu zako na ushupavu wa ujana wako basi (na yeye) atakufanyia wema katika kipindi cha utuuzima wako .
المصدر :
من المجلس الخامس من مجالس تعليق على سنن أبي داوود
Maelezo ya mfasiri:
Ni nasaha zenye thamani kwa wanandoa kutoka kwa sheikh -Allah amuhifadhi- na mimi nitazifafanua kwa nukta zifuatazo :
1- Mke anatakiwa ajue kuwa pindi mumewe anapoacha kutekeleza haki zake kwake hilo analolifanya ni dhulma na huo ni uovu lakini hilo lisimpelekee huyo mke kulipiza kisasi na yeye akaacha kumtekelezea mumewe haki zake na akajiingiza katika madhambi bali anatakiwa asubiri na kumpa nasaha kwa njia mbalimbali hata kwa kuwatumia watu wenye hekima kama masheikh n.k .
2- Mume anatakiwa afumbie macho makosa ya mkewe kwa sababu maumbile ya wanawake yapo hivyo asili ya maumbile yao ni hivyo hautopata mke aliyenyooka, isipokuwa makosa madogo madogo ni kuyaacha tu na kuyapuuza ama ukifuatilia kila kosa basi hautompata mke unayemtaka katu na kila siku utaoa na kuacha .
3- Na mke pia afumbie macho yale yanayomkera kutoka kwa mumewe kwa sababu kufanya hivyo ni ni sababu ya kuishi maisha ya raha na utulivu na moyo na kuwa na afya njema kwa sababu baadhi ya magonjwa husababishwa na msongo wa mawazo .
4- Tunatakiwa tumuige Mtume wetu -swala na salamu za Allah zimfikie-yeye alikuwa na subira ya kipekee katika kuishi na wakeze mpaka yanapotokea yale yenye kutokea huyatatua kwa njia ya hekima na busara na wala hatumii nguvu na jazba .
5- Mwisho mume unatakiwa ukumbuke kuwa kama Allah-aliyetukuka-atakupa umri mrefu hakuna atakayekusaidia na kukuchunga muda ambao haujiwezi isipokuwa mkeo au wakezo na kama utakuwa umemfanyia wema mkeo katika kipindi cha ujana wako na nguvu zako basi huyo mkeo atakufanyia wema kipindi cha uzee wako muda ambao haujiwezi na kumbuka kuwa muda huo watoto wako wote wakiume na wakike hata kama watakuwa wanakufanyia wema kiasi gani lakini hawatoweza kukutunza na kukuhudumia kama mkeo kwa sababu kuna huduma ambazo pengine zinamuhitajia mke pekee .
Ni nasaha zenye faida kubwa kwa wenye kuzingatia .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa:Shabani 1, 1443H ≈ Feb 21, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•