Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
قال رجلٌ لِأُوَيْسَ الْقَرَنِي- رحمه الله تعالى- :
صلنا يا أويس بالزيارة
Kuna mtu alimwambia Uwais Al-Qaraniy- Allah aliyetukuka amrahamu- :
Tuunge ewe Uwais kwa kututembelea
فقال له : قد وصلتك بما هو خير من الزيارة واللقاء وهو الدعاء بظهر الغيب
Basi (Uwais) akamwambi: Hakika nimekuungeni kwa lile ambalo ni bora zaidi ya kukutembeleeni na kukutana , nako ni (kukuombeeni) dua (hali) hampo
إن الزيارة واللقاء ينقطعان
والدعاء يبقى ثوابه
Bila shaka kutembeleana na kukutana kunakatika (kuna ukomo) ,na dua thawabu zake zinabaki .
📚تاريخ دمشق لابن عساكر ٤٤٩/٩
Maelezo ya mtarjumu:
Muislamu anatakiwa awaunge jamaa zake na ndugu zake waislamu kwa kuwafanyia ziara yaani kuwatembelea ,na kumekuja hadithi nyingi zinazoonesha ubora wa kumtembelea ndugu yako muislamu , lakini hapa tunaona Uwaisu Al-Qaraniy -Allah amrahamu- aliwaambia hawa watu pindi walipomwambia : Unga mahusiano yetu kwa kututembelea ,akawajibu kuwa yeye anaunga mahusiano yao kwa kulifanya lilokuwa bora zaidi kuliko hilo la kuwatembelea nalo ni kuwaombea dua hali ya kuwa wako mbali na yeye, na tendo hili lina ubora kama ilivyothibiti kutoka kwa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie-.
عن أبي الدرداء – رضي الله عنه – عن النبي -صلى الله عليه وسلم قال :
Kutoka kwa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – amesema:
دعوة المرء المسلم لأخيه بظهر الغيب مستجابة،عند رأسه ملك،
Dua ya mtu muislamu kwa ndugu yake kwa ghaibu (hali ya kuwa hayupo) ni yenye kujibiwa,
mbele ya kichwa chake (muombaji) kuna malaika,
كلما دعا له بخير قال الملك الموكل به: آمين
Kila anapomuombea (ndugu yake) ya kheri, husema (yule) Malaika aliyewakilishwa kwa hilo:
Ewe Allah jibu maombi haya,
ولك بمثل.
Na wewe (muombaji) upate mfano (wa uliloomba).
📚 صحيح مسلم (٢٧٣٢)
[ Swahih Muslim (2733) ]
Maana ya hadithi:
Kumuombea dua ndugu yako muislamu katika hali ambayo hayupo tendo hili hujulisha imani ya kweli kwa sababu Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie -amesema:
” لا يؤمن أحدكم حتى يحب لأخيه ما يحب لنفسه “
“ Hatokuwa muumini wa kweli mmoja wenu, mpaka ampendelee ndugu yake yale anayoyapendelea nafsi yake ”
Basi unapomuombea dua ndugu yako hali ya kuwa yupo mbali na wewe na ukamuombea dua bila ya kukuusia ufanye hivyo hii ni alama kuwa wewe unampendelea ndugu yako yale unayoipendelea nafsi yako,
Na kuwaombea dua waumini ambao wapo mbali hata kama hauwafahamu ni katika utaratibu wa mitume kama alivyosema Ibrahim -Swala na salamu za Allah zimfikie:
” ربنا اغفرلي ولوالدي وللمؤمنين يوم يقوم الحساب “
“Mola wetu Mlezi !Nisamehe mimi na unistiri na wazazi wangu wawili na waumini ;siku ya kusimama hisabu (Kiama) ” .
Hapa Ibrahimu – swala na salamu za Allah zimfikie – amewaombea waumini wote, na sisi tunawaombea ndugu zetu katika swala zetu hali ya kuwa hawapo au wapo mbali kila mmoja katika sisi husema:
” السلام علينا وعلى عباد الله الصالحين “
“Amani iwe juu yetu, na juu ya waja wema wa Allah”
Na Mtume – swala na salamu za Allah amesema – pindi tunaposoma dua hii basi humfikia kila mja mwema mbinguni na ardhini.
Huu ndiyo ubora wa kumuombea dua ndugu yako hali ya kuwa hayupo au yupo mbali na wewe, lakini asiwe amekuomba umuombee dua kwa sababu ikiwa amekuomba umuombee anakuwa kana kwamba yupo pale unapomuombea kwa sababu yeye alikuomba, ama ukimuombea bila ya yeye kukwambia au kukuomba niombee hapo ndipo kunapatikana malipo haya na fadhila hizi za kuwakilishiwa Malaika na kukuombea.
Tanbih: Maneno haya nimeyachukua katika Sher’he ya Riyaadh Sswalihiin ya Ibn ‘Uthaimin – Allah amrahamu – pamoja na kuongeza na kupunguza baadhi ya sehemu ili tarjama ikae sawa.
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Swafar(Mfungo tano) 12, 1443H ≈ September 19, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•