Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
NI SUNNA KUFUNGA MASIKU TISA YOTE YA MWANZO YA MWEZI WA MFUNGO TATU
قَالَ العلّامــة ابنُ عُثَيـمِين – رَحِمهُ الله –
Amesema mwanachuoni mkubwa ibn ‘Uthaimin – Allah amrahamu –
صيام العشر من ذي الحجة من الأعمال الصالحة ولا شك، وقد قال النبي – ﷺ –
Kufunga (masiku) kumi ya mwanzo ya Mfungo tatu ni katika matendo mema na hakuna shaka na hakika amesema Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie –
{ ما من أيام العمل الصالح فيهن أحب إلى الله من هذه العشر »
قالوا: يا رسول الله، ولا الجهاد في سبيل الله؟ قال: « ولا الجهاد في سبيل الله، إلا رجل خرج بنفسه وماله فلم يرجع من ذلك بشيء }
{ Hakuna katika masiku (ambayo) matendo mema hupendeza zaidi kwa Allah kuliko masiku haya kumi, (Maswahaba – Allah awaridhie) wakasema: Ewe mjumbe hata kuipigania dini ya Allah akasema (Mtume): Na wala (hazilingani na) kuipigania dini ya Allah, isipokuwa mtu (ambaye) ametoka yeye mwenyewe na mali yake, na hakikurudi katika hivyo chochote (yaani akafa na mali yake ikateketea) }
فيكون الصيام داخلا في عموم هذا الحديث على أنه ورد حديث في السنن حسنه بعضهم, أن الرسول -ﷺ- كان يصوم هذه العشر، يعني ماعدا يوم العيد، وقد أخذ به الإمام أحمد بن حنبل رحمه الله والصحيح أن صيامها سنة.
Basi inakuwa funga ni yenye kuingia katika ujumla wa hadithi hii, juu ya kuwa (pia) imekuja hadithi katika (vitabu vya) sunan na baadhi ya (wanachuoni) wamehukumu kuwa ni hadithi hasan kwamba Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – alikuwa akifunga hizi siku kumi kwa maana (siku tisa) ukiondoa siku ya eid na bila shaka ameichukua hiyo (hadithi) Imamu Ahmad – Allah amrahamu – na sahihi ni kuwa kufunga (masiku) hayo ni sunna.
مجموع الفتاوى والرسائل (٢٠ /٤٣)
Maelezo:
Hadithi aliyoiashiria Sheikh ni hii aliyoitaja Abuu Daud (2437)
عن هُنَيْدَةَ بن خالد رضي الله عنه عن امرأته عن بعض أزواج النبي صلى الله عليه وسلم – رضي الله عن الجميع قالت:
Kutoka kwa Hunaidah bin Khalid – Allah amridhie – kutoka kwa mkewe kutoka kwa baadhi ya wake wa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie: Allah awaridhie wote (huyo mke wa Mtume) amesema:
كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَصُومُ تِسْعَ ذِي الْحِجَّةِ, وَيَوْمَ عَاشُورَاءَ وَثَلَاثَةَ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ.
Alikuwa mjumbe wa Allah – swala na salamu za Allah zimfikie – akifunga siku tisa za (mwanzo) za Mfungo tatu na siku ya ‘Ashuraa na siku tatu kila mwezi.
قال الشيخ الألباني – رحمه الله: إسناده صحيح
Akasema Sheikh Al-baaniy – Allah amrahamu – Sanadi yake ni sahihi
Maelezo ya mfasiri :
Hii hadithi ni dalili ya usuna wa kufunga siku hizi tisa, ama hadithi ya mama Aisha – Allah amridhie – inayosema kuwa Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – hakufunga masiku haya, wanachuoni wanasema kuwa:
المثبت مقدم على النافي, من علم حجة على من لم يعلم
Mwenye kuthibitisha anatangulizwa juu ya mwenye kukanusha, aliyejua ana hoja juu ya yule asiyejua. Na pia huwenda Mtume aliacha kufunga baadhi ya muda kwa sababu ya safari, maradhi au shughuli.
Tanbihi:
Kuna wanachuoni wanaidhoofisha hadithi hiyo ya kufunga masiku tisa yote, lakini hata kama hadithi itakuwa dhaifu itabakia funga kuwa inaingia katika matendo bora ambayo yanatakiwa yakithirishwe katika masiku haya, kwa ajili hii amesema imamu Annawawiy – Allah amrahamu- kuhusu kufunga katika masiku haya:
” صيامها مستحب استحبابا شديدا “
” Funga yake ni yenye kusuniwa mno “
📚 شرح النووي على صحيح مسلم (٣٢٠/٨)
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Iliandaliwa: Dhul-Qaadah 30, 1441H ≈ July 21, 2020M, ikarudiwa kurushwa :Dhul-Qaadah 29,1442H≠ Jul 9,2021M
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
Shukran