NJIA YA KUPATA FURAHA KATIKA NDOA

Kupata darasa za ndoa jiunge nasi telegram kwa link hii: ⬇️
https://t.me/Darasazandoa

https://t.me/fawaidussalafiyatz

NJIA YA KUPATA FURAHA KATIKA NDOA

قال العلامة ابن عثيمين – رحمه الله في ((الشرح الممتع )) (12/ 383):

وينبغي للإنسان في معاشرته لزوجته بالمعروف أن لا يقصد السعادة الدنيوية، والأنس والمتعة فقط، بل ينوي مع ذلك التقرب إلى الله ـ تعالى ـ بفعل ما يجب، وهذا أمر نغفل عنه كثيرا، فكثير من الناس في معاشرته لزوجته بالمعروف، قصده أن تدوم العشرة بينهما على الوجه الأكمل. ويغيب عن ذهنه أن يفعل ذلك تقربا إلى الله تعالى، وهذا كثيرا ما ينساه، ينسيه إياه الشياطين، وعلى هذا فينبغي أن تنوي بهذا أنك قائم بأمر الله:

Amesema mwanachuoni mkubwa ibn ‘Uthaimin- Allah amrahamu – katika sher’he l-mumti’i (12/383):

Na inatakikana mwanadamu katika kuishi na mkewe kwa wema asikusudie raha ya dunia na maliwazo na starehe pekee, bali anuie pamoja na hayo kujikurubisha kwa Allah – aliyetukuka – kwa kufanya yale yanayowajibika na hili ni jambo wanaloghafilika nalo wengi, basi wengi katika watu (utamkuta mmoja) wao katika kuishi na mke wake kwa wema, makusudio yake ni kudumu maisha baina yao kwa sura ya ukamilifu zaidi. Na kunatoka akilini mwake kulifanya hilo kwa kujikurubisha kwa Allah – aliyetukuka – na hili mara nyingi (mume) hulisahau, Shetani humsahaulisha na juu ya hili (tulilolizungumza) basi inatakikana unuie kwa hili (unalolifanya) kuwa wewe unatekeleza amri ya Allah:

{ وعاشروهن بالمعروف }

{ Na ishini nao kwa wema }

وإذا نويت ذلك حصل لك الأمر الثاني؛ وهو دوام العشرة الطيبة، والمعاملة الطيبة، وكذلك بالنسبة للزوجة.

Na utakaponuia hilo litapatikana kwako jambo la pili; Nalo ni kudumu maisha mazuri na muamala mzuri na vile vile kwa mnasaba wa mke (anuie hili pia).

Maelezo ya Mfasiri:

Mume anatakiwa aweke nia ya ibada katika kila wajibu anaomfanyia mkewe kama vile kumlisha, kumvisha, kumpa makazi yote haya anatakiwa aweke nia ya ibada na hapa ndipo atakuwa anatekeleza amri aliyoimrisha Allah – aliyetukuka – ya kuishi na wanawake kwa wema na kama mume atakusudia ibada bila shaka wanandoa hao wataishi maisha mazuri kwa sababu kama atanuia ibada basi hatochoka kufanya wema na hata kama kuna kasoro anaziona kutoka kwa mkewe hazitomfanya asiendelee kumfanyia wema mkewe kwa sababu anajua kuwa yupo katika ibada na Allah atamlipa. Na vile vile mke nae anuie ibada kwa yale anayomtekelezea mumewe wanandoa wote wakiwa hivi basi bila shaka wataishi maisha ya raha na furaha.

Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 05 – Rabi’u-Awwal – 1442H ≈ 22 – October – 2020M. Ikarudiwa kurushwa Dhul-Qaadah 24-1442= 4 -July -2021M
Tembelea website yetu: ⇩⇩
https://www.fawaidusalafiya.net

Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Kupata darasa za ndoa jiunge nasi Telegram kwa kubonyeza link hii:
https://t.me/Darasazandoa

Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *