NJIA YA MWANAMKE KUPATA DARAJA KUBWA PEPONI NA KUPENDWA NA MUMEWE.

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

كتب الشيخ محمد بازمول -حفظه الله-:

Ameandika sheikh Muhammad Bazamul- Allah amuhifadhi-:

المرأة لا تعرف مقدار المكانة العظيمة التي تكون لها عند الله تعالى بإحسانها إلى زوجها!

Mwanamke hajui kiwango cha daraja kubwa ambalo atakuwa nalo mbele ya Allah -aliyetukuka-kwa kumfanyia ihsani mumewe!

لا تعلم مقدار المحل الذي تكون فيه من قلب زوجها لما تفعل ذلك!
Na wala hajui kiwango cha sehemu anayokuwa ndani yake katika moyo wa mumewe pindi anapolifanya hilo !

فاجعلي بيتك سكنا لزوجك ، ساعديه في إذهاب الهم والحزن، و لا تكوني أنت سبب حزنه وقلقه.

Basi ifanye nyumba yako ni utulivu kwa mumeo,msaidie katika kuondosha msongo wa mawazo na huzuni ,na wala wewe usiwe ni sababu ya kuhuzunika kwake na kupata kero.

املأي بيتك رفقا وودا ليملأه زوجك لك حبا واحتراما وحنانا.

(Wewe mke) ijaze nyumba yako upole na mapenzi ya hali ya juu ili mumeo aujaze (moyo) wake kwako mapenzi ,na heshima na mahaba makubwa .

بارك الله لكما وعليكما وجمع بينكما في خير.

Allah awape baraka (katika ndoa yenu) na awabariki (katika kizazi) na akukusanyeni katika heri.

من الموقع الرسمي للشيخ (فيس بوك)

Maelezo ya mfasiri :

Mke kumfanyia ihsani mumewe ni jambo lenye ujira mkubwa mbele ya Allah kwa huyu mwanamke na ni sababu katika sababu za kuingia peponi kama ilivyokuja katika hadith, na pia mke anapomfanyia ihsani mumewe ajue kuwa ndiyo sababu ya huyo mume, kumpenda na kuzidisha mahaba kwake :

Pindi mke atakapoifanya nyumba ni sehemu ya utulivu kwa mumewe, na akawa, ndiyo sababu ya kuondosha huzuni na msongo wa mawazo wa mumewe na akajiepusha kuwa ni sababu ya mumewe kuwa na huzuni na kukereka .

Awe mpole kwa mumewe na mwenye mapenzi na kama mke akiwa hivi basi atapata mapenzi na mahaba ya hali ya juu kutoka kwa mumewe na heshima pia.

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa : Mfungo nane 8, 1443H ≈ Dec 12, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *