Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
🔊 NJIA YA MWANAMKE YA KUJIKINGA NA FITNA 💫
✍🏻قــال الشيخ ابن عثيمين رحمه الله تعالى :
Amesema sheikh ibn Uthaimin- Allah aliyetukuka amrehemu-:
إن المرأة التي تقول إن بقاء المرأة في بيتها سجن
أقول :إنها معترضة على قول الله تعالى :
Hakika mwanamke ambaye anasema :
” Bila shaka mwanamke kubakia nyumbani kwake ni kifungo/gereza ” .
(Mimi) nasema : Hakika huyo (mwanamke) anapingana na kauli yake Allah aliyetukuka-:
(وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ)
كيف نجعل ما أمر الله به سجناً ؟
{Na tulizaneni majumbani mwenu},
vipi tulifanye lile aliloamrisha Allah ni kifungo (gereza) ?
لكنه سجنٌ على من تُريد التبذل والالتحاق بالرجال ،
lakini hicho ni kifungo kwa yule anayetaka kujiachia ,na kukutana na wanaume,
وإلا فإن سرور البقاء في البيت هو السرور وهو الحياء ، وهو الحشمة ، وهو البعد عن الفتنة .
na kama (si hivyo) basi bila shaka furaha ya (mwanamke) ni kubakia nyumbani , hiyo ndiyo furaha halisi na hiyo ndiyo (sifa ya) kuwa na aibu ,na hiyo ndiyo heshima na huko ni kujiweka mbali na fitna .
▪فتاوى نورعلى الدرب شريط رقم ٣٧١
Maelezo ya mtarjumu:
Mwanamke kutulizana nyumbani ni amri ya Allah ,na nyumba kwa mwanamke :
Ndiyo ofisi yake, na ndiyo kituo chake cha kufanyia kazi na ndiyo sehemu ya kumuhifadhi na kumlinda kutokana na mbwa mwitu wa kibinadamu ,na mwanamke anapotoka nyumbani akaenda kufanya kazi haswa kazi za mchanganyiko baina ya wanawake na wanaume basi hapo subiri mabalaa ,na maovu yatakayokithiri katika jamii na pia familia ni lazima zikose maadili kwa sababu zimekosa mlezi ambaye ni mama.
Mtarjumu: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 9, 1443H ≈ October 15, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•