Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
makala namba ( 1)
◾️ قال العلامة ابن عثيمين رحمه الله:
Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimin- Allah amrehemu-:
الخشوع في الصلاة هو حضور القلب، ومما يعين عليه:
Unyenyekevu katika swala ni kuuhudhurisha moyo, na yale yanayosaidia huko (kuhudhurisha moyo):
ما أرشد إليه النبي ﷺ حيث شُكي إليه أن الرجل يأتيه الشيطان يوسوس له في صلاته,ويحول بينه وبين صلاته.
(mfano) ule muongozo alioutoa Mtume -swala na salam za Allah ziwe juu yake- pale aliposhitakiwa kwamba kuna mtu (ambaye) Shetani humjia na kumtia wasiwasi katika swala yake,
na huweka kizuizi baina yake na swala yake ,
فأمر النبي ﷺ ، أن يتفل الرجل على يساره ثلاث مرات، ويستعيذ بالله من الشيطان الرجيم ، هذا من أنفع الأدوية.
basi Mtume -swala na salam za Allah ziwe juu yake- akamuamrisha apulize upulizaji unaoambatana na mvuke mvuke wa mate kidogo, upande wake wa kushoto mara tatu,na ajikinge kwa Allah kutokana na Shetani aliyefukuzwa mbali na rehma za Allah.
Hii ndio dawa yenye manufaa zaidi.
ومنها أيضا: أن يستحضر الإنسان عظمة من هو واقف بين يديه وهو الله عز وجل
Na miongoni mwa hizo (njia za kupata unyenyekevu) : Ni mtu kuhudhurisha ukubwa wa yule aliyesimama mbele yake naye ni Allah- aliyeshinda na kutukuka- ,
ويقبل على صلاته، يتدبر ما يقول من كلام الله، وما يقول من ذكر، وما يفعله من أفعال و حرکات؛
Na aielekee -swala yake yake ,azingatie yale anayoyasoma katika maneno ya Allah,na yale anayoyasema katika nyiradi,na yale anayoyafanya katika vitendo na harakati (mbalimbali);
حتى تتبين له عظمة الصلاة، وحينئذ تزول عنه هذه الوساوس، وجرّب .
(ayafanye haya) mpaka umbainikie utukufu wa swala, wakati huo utamuondoka huu wasiwasi , na (wewe) jaribu (hili utaona).
📚 دروس وفتاوى الحرمين( ١٣/٢٦٦).
Maelezo ya mpitiaji:
Swala ambayo haina unyenyekevu ni kama vile ukachukua mtumwa aliyefariki au kijakazi aliyefariki ukampelekea zawadi mfalme !bila shaka swala isiyokuwa na unyenyekevu ndani yake Allah haikubali pamoja na kwamba mswaliji atakuwa ametimiza wajibu wa swala hiyo lakini thawabu hatopata ,kwa sababu mja hulipwa katika swala yake kwa kadri ya unyenyekevu wake ndani ya swala.
انظر : الوابل الصيب.
Tanbih:
Mtu anapokuwa anaswali msikitini katika jamaa kisha akajiwa na wasi wasi ,ni vipi atapuliza na kutema vijimate kushotoni kwake ?
Swali hili amelijibu -ibn Uthaimin- Allah amrahamu-:
“Kama akiwa ni mtu wa mwisho upande wa kushoto anaweza kutema vijimate nje ya msikiti ,kama si hivyo basi ateme katika nguo yake au kilemba chake au kitambaa chake ,na kama halikuwepesika hili (pia) basi inatosha kugeuka kushotoni kwake na aseme:
أعوذ بالله من الشيطان الرجيم
Najikinga kwa Allah kutokana na Shetani aliyetengwa mbali na rehema za Allah.
فتاوى نور على الدرب : ١٥٥/١٢.
Na vile vile amesema sheikh -Allah amrahamu-:
Pindi mtu anapokuwa katika jamaa afanye nini ? vipi atapuliza na kutema vijimate kushotoni kwake mara tatu? .
Inatosha kujikinga kwa Allah kutokana na Shetani aliyetengwa mbali na rehema za Allah bila ya kupuliza na kutema vijimate ili usimuudhi aliyekuwa pembeni mwako .
فناوى نور على الدرب : ١٨٥/٤٥
Mpitiaji: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 27, 1443H ≈ Oct 4, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•