NYIRADI KWA ANAYEONA VITISHO USINGIZINI.

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

جاء رجلٌ إلى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فشكا إليه أهاويلَ يراها في المنام،فقال :

(Kuna) mtu alikuja kwa Mtume -swala na salam za Allah ziwe juu yake- akamshitakia vitisho anavyoviona usingizini ,basi (Mtume)-swala na salamu za Allah zimfikie- akasema:

“إذا أَوَيتَ إلى فراشك فقل: أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللهِ التَّامَّةِ مِنْ غَضَبِهِ وَعِقَابِهِ، وَمِن شَرِّ عِبَادِهِ، وَمِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ وَأَنْ يَحْضُرُونِ”

“Pindi utatakapokiendea kitanda chako basi sema (maneno haya):

Najikinga kwa maneno ya Allah yaliyotimia kutokana na hasira zake na adhabu zake, na kutokana na shari za waja wake, na kutokana na wasiwasi wa mashetani wasije kunihudhuria “

سلسلة الصحيحة للألبانى:
(رقم ٢٦٤)

Maelezo ya mpitiaji:

Hii ni dua tukufu ambayo Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- alimpa muongozo yule aliyekuwa akipatwa na hofu usingizini mwake kwa sababu ya yale aliyokuwa akiyaona usingizini mwake akisema maneno haya basi itakuwa ni sababu ya kuondoka hofu na mfazaiko na atapata utulivu katika usingizi wake na hofu itaondoka kwake .

Na hii ni dua tukufu na yenye baraka : Mja anatangaza katika dua hii kukimbilia kwake kwa Allah kutokana na ghadhabu zake (Allah) na adhabu zake na kutokana shari za waja wake na kutokana na shari za Mashetani wasimhudhurie usingizini mwake na katika hali zake zote , na Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- ameeleza kuwa mwenye kusema maneno hayo Mashetani hawatomdhuru bali atasalimika nao .

Muumini anakimbilia kwa Allah kutokana na kila kinachomuudhi kwa sababu anajua kuwa Allah ndiye anayepanga na kukadiria yote ya viumbe.

Na vile vile faida tunayopata hapa :Maneno ya Allah yametimia hayapatwi na mapungufu wala kasoro kama yalivyo maneno ya viumbe .

Vile vile tunapata faida kuwa :Kukasirika ni sifa ya kivitendo inayothibiti kwa Allah -aliyetukuka-, Allah ameisifu nafsi yake kwa sifa hiyo katika kitabu chake na Mtume wake-swala na salamu za Allah zimfikie- amemsifu Allah na sifa hiyo katika hadithi zake , Na Allah anakasirika na anaridhia na anapenda na anaghadhibika ,na anasifa nyingi za kivitendo zilizokuja katika qurani ,na sifa hizi tunamthibitishia Allah kwa vile inavyonasibiana na utukufu wake bila ya kumfananisha ,wala kubadilisha na kupindua, na wala kukataa kuthibitisha .

Pia tumepata faida kuwa maneno ya Allah si kiumbe bali ni sifa katika sifa zake na ndio maana tunaruhusiwa kujikinga kwa maneno ya Allah , na kujikinga kwa kiumbe ni ushirikina.

Angalia:

فقه الأدعية والأذكار ، للشيخ عبد الرزاق البدر – حفظه الله –

Mpitiaji: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Swafar/ Mfungo tano 29, 1443H ≈ Oct 6, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *