Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
دار البرزخ
NYUMBA YA MAISHA BAADA YA KIFO
🎙 قال العلامة صالح الفوزان-حفظه الله:
AMESEMA MWANACHUONI MKUBWA SWAALIH AL – FAUZAN -ALLAH AMHIFADHI- :
وهي دار القبور برزخ بين الدنيا والآخرة والبرزخ معناه الفاصل والحياة بالقبور تسمى بالحياة البرزخية وفيها عجائب فيها نعيم أو عذاب إما حفرة من حفر النار أو روضة من رياض الجنة
ويبقى الأموات في قبورهم إلى أن يشاء الله جل وعلا بعثهم وحشرهم للحساب والجزاء
وهذه الدار محطة الانتظار .
“Hiyo ni nyumba ya makaburi ni kizuizi baina ya dunia na akhera na barzakh maana yake ni kizuizi na maisha ndani ya makaburi huitwa maisha ya kizuizini
na ndani yake kuna maajabu ndani yake kuna neema au adhabu ima (nyumba hiyo) ni shimo miongoni mwa mashimo ya motoni au bustani miongoni mwa mabustani ya peponi
na maiti watabaki katika makaburi yao mpaka (pale) Allah -aliyetukuka na aliyejuu-atapotaka kuwafufua na kuwakusanya kwa ajili ya hesabu na malipo na nyumba hii (ya kizuizini) ni kituo (terminal) cha kusubiri.
📚 MAREJEO: ⇣
{{إعانة المستفيد ص٦٧ }} طبعة الرسالة العالمية.
[ I’aanatu l-mustafiid 67 ]
Chapa ya arrisaalutu l-a’alamiyyah
Maelezo:
Maisha ya kaburini ni marefu sana yanaanza pale mwanadamu atapofariki tu ,kama alivyoeleza Allah
ۖ وَمِن وَرَائِهِم بَرْزَخٌ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ
Na mbele yao kuna kizuizi (maisha baadaya kufa) mpaka siku watakapofufuliwa
المؤمنون (١٠٠)
Kaburini ni sehemu inayotisha mno na kuogopesha ndiyo maana maswahaba walipolijua hili walipatwa na hofu ya hali ya juu ,kama ilivyothibiti kutoka Uthman- Allah amridhie- :
عن هانئ مولى عثمان رضي الله عنهما قال:
Kutoka kwa Haani (aliyekuwa) mtumwa wa Athuman kisha akampa uhuru wake – (alisimulia) akasema:
((كان عثمان إذا وقف على قبر بكى حتى يبلَّ لحيته، فقيل له: تذكر الجنة والنار فلا تبكي، وتبكي من هذا؟
Alikuwa Athman anaposimama pembeni mwa kaburi hulia mpaka akaloesha ndevu zake ,basi (kuna siku) aliulizwa : (Vipi) unaikumbuka pepo na moto (lakini) haulii ,na unalia kutokana na (kuliona ) hili (kaburi) ?
فقال: إن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: القبر أول منازل الآخرة، فإن يَنجُ منه، فما بعده أيسر منه، وإن لم يَنجُ منه، فما بعده أشد منه)).
Basi (Athman) akajibu : Hakika Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie amesema -:
Kaburi ni makazi ya mwanzo ya akhera ,kama ataokoka humo (Kaburini) basi yale ya baadaye ni mepesi kwake ,na kama hakuokoka humo (kaburini) basi yale ya baadaye ni mazito zaidi ya hayo ya (kaburini).
رواه الترمذي .
Maana ya maneno ya Athuman -Allah amridhie- :
“Kama mtu ataokoka kaburini kutokana na adhabu ya kaburi basi yale yanayokuja mbele yake ni mepesi kwa sababu lau huyu muislamu angekuwa na madhambi basi yangefutwa kwa kuadhibiwa kaburini ,na kama hakuokoka na adhabu ya kaburi na hayakufutwa madhambi yake kwa adhabu ya Kaburi basi yale yanayomuelekea ni mazito zaidi .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: iliandaliwa August 22,2017. Na ikahakikiwa na kurushwa tena Shawwal 5, 1442H ≈ May 17, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•