Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
OA EWE MWANAFUNZI !
قال الشيخ ابن عثيمين -رحمه الله- :
Amesema sheikh ibn Uthaimin- Allah amrahamu-:
الزواج لا يعوق عن طلب العلم
بل ربما يعين على طلب العلم
قد يوفق الإنسان لإمرأة تقرأ وتكتب وتساعده
Ndoa haizuii kutafuta elimu bali huwenda ikasaidia juu ya kutafuta elimu,huwenda mwanadamu akapewa taufiq ya (kumpata) mwanamke anaye (weza) kusoma na kuandika (akawa) anamsaidia huyo (mumewe ktk kusoma) ,
فإن لم تكن فأقل مايكون أن يذهب عنه الوساوس والتفكير في الزواج
فالزواج يعين على طلب العلم
na kama (mwanamke) hakuwa (hivyo) basi kwa uchache itavyokuwa ni (kijana) kumuondoka wasiwasi na kufikiria ndoa ,basi (ikiwa hivyo) kuoa husaidia (katika) kutafuta elimu
وإذا كان أبوه يريد أن يزوجه فلا يرفض،فخير البر عاجله
na pindi baba wa huyo (mwanafunzi) atapotaka kumuozesha basi asikatae , na wema uliokuwa bora ni ule unaoharakishwa.
لقاء الباب المفتوح ٤٨
Maelezo ya mtarjumu:
Kutafuta elimu hakuzuii kuoa ,bali huwenda kuoa kukawa ndio msaada wa kutafuta elimu na haswa pindi atakapooa mwanamke mwenye kujua kusoma na kuandika kama alivyosema sheikh -Allah amrahamu- na bila shaka Allah akikujaalia mke anayekusaidia katika mambo ya akhera hakika umemiliki hazina kubwa mno , na imethibiti kuwa maswahaba -Allah awaridhie- walimuuliza Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- ni kitu gani wakimiliki ? Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – akawajibu:
لِيَتَّخِذْ أحدُكم قلبًا شاكرًا ، ولسانًا ذاكِرًا ، وزوجةً مؤمنةً ، تُعِينُهُ علَى أمرِ الآخرَةِ
Amiliki mmoja wenu moyo wenye kushukuru, na ulimi wenye kumtaja (Allah),na mke muumini anayemsaidia juu ya mambo ya akhera .
صحيح الجامع (٥٣٥٥).
bila shaka ukimpata mke anayekusaidia katika mambo ya ibada kama vile swala,funga, kufanya mema kwa ujumla na kujiepusha na maovu ,na ukipata mke mwenye dini ambaye anakusaidia katika kutafuta elimu ya dini yako basi hiyo ni nuru juu ya nuru .
Lakini hata kama haujapata mke anayejua kusoma na kuandika lugha ya kiarabu lakini ukampata mwenye dini bila shaka katika ndoa kuna utulivu wa nafsi na kuondoa wasiwasi na mawazo ya kuoa, na hili litamfanya mwanafunzi atafute elimu kwa utulivu pia.
Tanbih:
Unapotaka kuoa baada ya kumuelekea Allah fanya kila juhudi ya kupata mke mwema mwenye dini ,kwa sababu huwenda ukaoa mwanamke muovu ambaye akawa ndio sababu ya mtu kuacha kuisoma dini yake na kuharibikiwa katika dini.
Tunamuomba Allah salama.
Mtarjumu: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 22, 1443H ≈ October 28, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•