PAMBANA USIJE UKAIBIWA KITU HICHI KATIKA MAISHA YAKO.

قال ابن قيم الجوزية – رحمه الله- :

Amesema ibn l-Qayyim Al-jauziyyah -Allah amrahamu-:

دخل رجل على سهل بن عبد الله، فقال: «اللص دخل داري وأخذ متاعي.

Kuna mtu aliingia kwa Sahl bin Abdillah akasema : Kuna mwizi ameingia nyumbani kwangu na akachukua vitu vyangu .

فقال: اشكر الله، فلو دخل اللص قلبك – وهو الشيطان – وأفسد عليك التوحيد، ماذا كنت تصنع؟ !»

Basi (Sahl) akasema:

“ Mshukuru Allah ,lau angeingia mwizi wa moyo wako -naye ni Shetani- na angekuharibia tauhid ungefanya nini ?! ”

عدة الصابرين (ص ٢٩٢)

Maelezo ya mfasiri:

Ni bora uibiwe vitu vyako vyote ilivyo navyo kuliko kuibiwa tauhidi yako ,kwa sababu tauhidi maana yake ni kumpwekesha Allah yaani kumuabudia yeye pekee ,na yeyote atakayefariki hali hamuabudii Allah pekee kwa maana akafariki hali anamshirikisha Allah -aliyetukuka- basi mtu huyo makazi yake ni motoni milele na hakuna kitakachomsaidia mbele ya Allah -aliyetukuka- hata kama ana mali ,au akawa tajiri mkubwa na bilionea lakini maadamu hakumuabudia Allah pekee basi huyo ni mtu wa motoni milele .

Kama alivyosema Allah-aliyetukuka- pindi alipomzungumzia Abuu Lahb :

مَآ أَغْنَىٰ عَنْهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ

Hazitomsaidia mali zake na wala vile alivyovichuma .

المسد ٢

Na vile vile katika suratu l-Haqqah Allah -aliyetukuka- ameeleza maneno watakayoyazungumza makafiri siku ya kiama kwa njia ya kujuta miongoni mwa hayo ni :

مَا أَغْنَىٰ عَنِّي مَالِيَهْ ۜ

Hazikunisaidia mali zangu /hazikunikinga na adhabu.

الحاقة : ٢٨ .

Kwa hiyo kupoteza mali katika hii dunia ni kitu chepesi mno kwa muumini kuliko kupoteza tauhidi na uislamu na kuingia katika ukafiri au ushirikina na mwisho wake ni kukaa motoni milele.

Nasaha:

Tujitahidi kuzitunza imani zetu na kuilinda tauhidi yetu na tujiepushe na yale yanayoharibu tauhidi ya mtu au kuitia dosari ,kwa maana tujiepushe na ushirikina na ukafiri kwa sura zake zote.

Pia mshukuru Allah kwa neema ya uislamu ,neema ya kumpwekesha Allah na tambua kuwa hakuna neema kubwa zaidi ya neema ya tauhidi.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 21, 1443H ≈ Jan 24, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *